HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 4, 2018

ITC YA OBREY CHIRWA YATUA, TAYARI KUITUMIA AZAM FC


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Klabu ya Azam umeweka wazi kuwa usajili wa mshambuliaji mpya Obrey Chirwa umekamilika  kwa asilimia 100 baada ya Chama cha Soka nchini Misri (EFA) kuiachia Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa kuituma kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Nurdin Amin ‘Popat’, amesema kuwa tayari kibali hicho kimeshatumwa TFF na sasa wanachosubiri ni kukamilika kwa vibali vyake vya kufanya kazi nchini pamoja na leseni itakayomwezesha kucheza soka nchini.


EFA imeachia ITC yake baada ya Nogoom FC kuithibitishia kuwa wameachana na mchezaji huyo na yupo huru kujiunga na timu yoyote, ambapo wiki chache zilizopita Azam FC ilimaliza taratibu za kumuhamisha kwa kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja.


“Tunamshukuru Mungu jana jioni TFF imetupa taarifa ya kupokea ITC ya Chirwa kutoka Misri alipokuwa akicheza awali, hataweza kuiwahi mechi ya leo kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza ligi na kibali chake cha kufanya kazi kutokamilika, tunatarajia atacheza mechi ijayo ya Ijumaa dhidi ya Mbao,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad