HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 13 December 2018

Gulamali aachiwa huru, baada ya kukutwa hana kesi ya kujibu

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoa wa Singida imetupilia mbali kesi ya kupokea rushwa iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara, Haidar Hussein Gulamali baada ya kutopatikana na kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Consolata Singano baada ya upande wa Jamuhuri  kifungo kesi Kwani kutoa mashahidi 9. Na kusema amezingatia ushahidi wa mashahidi 9 wa upande wa Jamuhuri waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi was lakini kati yao wote  hakuna ushahidi unaomgusa Gulamali moja kwa moja.

Akisoma Uamuzi huo,  Hakimu Singano amesema upande wa mashtaka wameshindwa kuthibitisha kesi yao na kutoka Sababu moja wako Ni kutofautiana kwa mashahidi watatu kuhusu bahasha iliyobeba fedha.

Amesema katika ushahidi wao kila shahidi ametaja rangi tofauti ambapo mmoja ametaja Kaki, mwingine nyeupe, huku wa mwisho akitaja Brown jambo ambalo mahakama imeshindwa kuelewa bahasha ipi ilibeba fedha.

Pia amesema hata hatua za ukamataji hazikuanishwa vizuri kwani hakuna mahali iliyoonyesha Pesa ziliwahi kutaifishwa hadi zilipofikishwa mahakamani, pia namna zilivyotunzwa mpaka kufikishwa kama ushahidi.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Singano amesema anatupilia mbali kesi hiyo na kumuachia Huru a

Katika kesi hiyo Gulamali alikuwa akitetewa na wakili Godfrey Wasonga,  

Miongoni mwa mashahidi waliofika kutoa ushahidi mahakamani hapo Ni pamoja na  Ofisa Usalama mkoa wa Singida, Kiseo Nzowa anayedaiwa kupewa rushwa hiyo ambapo amedai anafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Shahidi huyo Katika ushahidi wake alidai Gulamali alimpa Sh.Milioni 2 ili amsaidie kupitisha jina lake kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Singida Kaskazini na kwamba yeye hakuwa Mjumbe Kamati ya Siasa Wilaya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad