HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 17, 2018

BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA

Na John Nditi, Morogoro
NAIBU Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema , Serikali inatarajia kufanya usanifu wa  barabara ya Morogoro- Dodoma yenye urefu wa kilometa zipatazo 259 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa ajili ya kupata michoro na gharama halisi ili kujengwa  upya kwa   viwango  cha ubora   na mahitaji ya sasa .

Naibu Waziri alisema hayo  mjini Morogoro  alipofanya ziara ya ukaguzi wa matengenezo ya barabara  katika maeneo mbalimbali kutoka Dodoma hadi Moropgoro  yakiwemo ya Kibaigwa , Gairo  na kuangalia shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa Magereza  barabara ya Morogoro- Dodoma .

Alisema , licha ya kuendelea kuihudumia   barabara kuu hiyo ,  kwa sasa Serikali imekuja na mpango mwingine wa kufanya usanifu kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 ili kupata michoro ambayo itaelezea  gharama halisi ya kujenga barabara mpya katika  kiwango cha ubora na mahitaji ya sasa.

Naibu Waziri alisema,  Serikali inatenga  fedha nyingi kila mwaka fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu ikiwemo ya Morogoro- Dodoma  ili ziweze  kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo ambapo kwa baabara hiyo iliyojengwa miaka zaidi ya 30 iliyopita kwa hali yake ya  sasa imechakaa  na kuzeeka.

Akizungumzia ujenzi wa mizani , Naibu Waziri alisema , Serikali itaendelea kujenga   mizani  ya kisasa katika barabara kuu nchini ambayo itapunguza  msongamano  wa magari  na  kuharakisha usafirishaji wa mizigo ,  abiria na pia  kulinda barabara .

Naibu Waziri alisema ,mizani ya kisasa inayojengwa na  iliyopo itakatoboreshwa ili ikidhi utoaji wa huduma zote   muhimu kama vituo vya Polisi, TRA, ukaguzi wa magari, upimaji wa ulevi kwa madereva , kuengesha magari na maeneo ya kupumzika madereva .

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga  alisema,  ujenzi  mzani hiyo ya  kisasa ulianza Oktoba 25, 2017  kwa gharama  ya  Sh  bilioni 14. 784 fedha zilizotolewa na Serikali kuu na hadi sasa  ujenzi wake umefikia  asilimia 70 na kiasi cha malipo kwa mkandarasi kilicholipwa ni Sh bilioni 5.7 sawa na asilimia 40.

Mhandisi Mtenga alisema  , mradi huo wa ujenzi wa mizani mbili za kisasa za kupima magari , eneo la Dakawa Magereza  una  majengo mawili  ya ofisi, vibanda viwili vya Polisi , vinne vya mlinzi na vyoo viwili na ni moja wapo ya hatua za kudhibiti na kupunguza uharibifu wa barabara kutokana na magari kuzindisha uzito.

 “ Hapa kutakuwa na mzani miwili mmoja  utapima magari yakiwa kwenye mwendo mdogo na utarekodi na kuhifadhi taarifa zote za gari husika  na gari itaruhusiwa kuendelea na safari iwapo hajazidisha uzito na ikiwa uzito umezidi litaelekezwa kwenda kupima kwenye mzani wa kawaida kwa uthibitisho” alisema Mtenga.

Hta hivyo alisema , ujenzi huo  ulipangwa ukiamilishwe ifikapo  Januari 24, 2019 , lakini kutoka na  kuchelewa  kupata eneo la upande mmoja wa  ujenzi   kwa zaidi ya miezi sita ambazo zilikuwa nje ya uwezo wa  mkandarasi  kutokana na ardhi kumilikiwa na Taasisi mbili tofauti za Serikali .

Mhandisi Mtenga alisema , kwa sasa mkandarasi wamewasilisha ombi la kuongezewa muda hadi Aprili 24, 2019,  na kwamba Wakala  utaendelea kumsimamia ili ujenzi huo ukamilishwe kwa wakati katika muda wa nyongeza ulioombwa.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akipata maelezo  ya   Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya  Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia) alipokagua  shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa  Magereza  barabara  kuu ya Morogoro- Dodoma  hivi karibuni na (  anayemfuatia Naibu Waziri ) ni Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti)  akisisitiza  jambo wakati akikagua shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa  Magereza  barabara  kuu ya Morogoro- Dodoma  hivi karibuni na ( wapili kushoto) ni Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akikagua  shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa  Magereza  barabara kuu ya Morogoro- Dodoma  hivi karibuni akiongozwa na  Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya  Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia)  akiambatana na  Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga ( wapili kushoto)  pamoja na Wakala wa Mradi kutoka Kampuni ya Group  Six International Ltd , Mhandisi Abdallah Rashid.( Picha na John Nditi).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad