HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 24 November 2018

ZAIDI YA MADEREVA 1600 WAPATIWA MAFUNZO ARUSHA

Na Vero Ignatus, Arusha
Madereva wa mabai ya kubebea abiria katika mkoa wa Arusha wamepatiwa mafunzo ilihali wengine waki3ndelea na mafunzo. Akizungumza Mrakibu wa polisi Joseph Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha amesema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa madereva wote wanapata elimu na wanatoa huduma inayoendana na elimu waliyoipata

Tangia kuanzishwa kwa mafunzo ya madereva miezi minne iliyopita madereva 1600 wamehitimu mafunzo wa magari ya kubeba abiria (PSV)kupitia chuo cha Veta pamoja na chuo rafiki wa NIT cha Moden driving vyote vya mkoa wa Arusha. "Pamoja na mapambano hayo ya ajali za barabarani ni lazima kuhakikisha kuwa wapo madereva wenye weledi" alisema Bukombe. 

Aidha amesema mafunzo haya yamesaidia sana kwani mkoa hapo pamekuwa salama bila Ajali. "Tangia tumeanzisha mafunzo takribani miezi minne iliyopita kwa mkoa wa Arusha tupo salama, na ukikuta ajali imesababishwa na bodaboda na siyo magari ya abiria" alisema Bukombe

Mara baada ya kuona ajali zimeongezeka jeshi la polisi liliendesha ukaguzi wa leseni na kugundua kuwa madereva wengi wana leseni lakini hawana vyeti, kwahiyo yamkini wanazipata leseni kwa njia wanazozijua wao. "Sisi tukasema hawawezi kuendelea na leseni walizonazo badala yake warudi darasani kwenda kusoma ili waweze kupata vyeti"alisema

Akizungumza wimbi la Magari ya viongozi wa serikali kupata ajali Bukombe amesema hakuna aliye juu ya sheria kwani hata madereva hao wameshaanza kushughulikiwa. "Mara ya kwanza ulipita tu kama upepo wa kuwasaha ulakini sasa unapoaona kitu kinazidi kuleta shida ule upepo tumeshafutilia mbali na wao wanachukuliwa hatua "alisema .Amesema Jeshi la polisi linafikiria ninamna gani wanaweza kushirikiana na wizara kuhakikisha madereva wao wanawapeleka mafunzoni

Aidha Bukombe ametoa wito kwa madereva wakaidi ambao hawaoni umuhimu wa kuingia darasani, wale ambao wanasubiri waone ninini hatima ya jambo hilo amewashauri kuw ni vyema wakarudi darasani kujisomea wasisibirie matokeo kwani jeshi la poisi hatitawafumbia macho. Bikombe amesema maelekezo hayo yalipoyolewa na serikali yalikuwa ni kwa minubu wa miezi mitatu ambapo zoezi hilo likikuwa limalizike tarehe 1 novemba 2018, ikaonekana vyuo vilelemewa na maderevya hivyo serikali ikaongeza hadi miezi miwili hivyo litamalizika januari mosi 2019

Ukaguzi wa leseni na vyeti utaendeshwa rasmi januari mosi 2019 hivyo madereva ambao watakutwa hawana leseni na vyeti sheria itafuata mkondo wake.

Mrakibu wa polisi Joseph Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad