HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 7 November 2018

WATAALAM WANAWAJIBU WA KUINGIZA UTAALAM KATIKA UCHUMI WA VIWANDA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO Kikuu Mzumbe kimesema watalaam katika sekta mbalimbali wanawajibu kuingiza uwezo wao katika uchumi wa viwanda ili kuendana na malengo ya serikali.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi wakati wa kikao cha maafisa rasilimali watu kilichofanyika Chuoni hapo, amesema watalaam katika kada mbalimbali wanahitaji kutambua na kufungua fursa katika sekta ya viwanda katika kuhakikisha nchi inafikia malengo.

Amesema kuwa Chuo kimekuwa kikiendesha Program katika kada zinazozalishwa katika chuo ili kuhakikisha watalaam wanapeleka ujuzi wao ambao utasaidia taifa kuvuka mipango yake ya kufika kwenye uchumi wa viwanda vya ndani.

Profesa Ngowi amesema kuwa maafisa Rasilimali watu wanawajibu wa kuhakikisha kila anayefanya kazi katika viwanda anapanda kutokana na taratibu zilizowekwa ili kukidhi mahitaji ya wafanyakazi.

Kwa upande wa Mratibu wa Program hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Dkt Faisal Issa amesema kuwa maafisa Rasilimali watu ni watu muhimu katika mapinduzi ya uchumi wa viwanda na usimamizi wa maslahi ya wafanyakazi kwa kufuata misingi iliyowekwa.

Issa amesema kuwa wafanyakazi wanatakiwa kupanda cheo ikiwa ni pamoja na kusimamia masilahi yao katika kuhakikisha viwanda hivyo vinazalisha na kufikia malengo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza katika kikao cha maafisa Rasilimali watu kilichofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Program za  kujengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe  Mhadhiri Dkt Faisal Issa akizungumza  kuhusiana na kikao hicho kwa maafisa rasilimali watu kilichofanyika Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam.
 Mwendeshaji wa Mdahalo wa Maafisa Rasilamali Watu Carl Bosser akitoa maalezo kuhusiana na mdahalo kwa maafisa kilichofanyika Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam.
 Meza kuu wakijibu maawali ya wadau mbalimbali
Picha ya Pamoja maafisa wa Rasilamali Watu na Watendaji wa Chuo Kikuu Mzumbe

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad