HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 1 November 2018

WANACHAMA MNIPE KURA KWA WINGI NIKAMALIZIE NILIPOISHIA- IDDY KAJUNA

Mgonbea wa nafasi ya Ukurugenzi wa Bodi ya Klabu ya Simba Iddy Kajuna alipokuwa anachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MGOMBEA wa nafasi ya .Ukurugenzi wa Bodi ya Klabu ya Simba Iddy Kajuna amesema anahitaji kurejea kwenye nafasi kuu ni kutaka kuendeleza pale apoishia.

Kajuna mpaka sasa ni Kaimu Makamu wa rais wa Klabu y Simba ameweka wazi nia yake kurejea katika uongozi wa Klabu hiyo ili kuendelea pale alipoishia.

Akizungumza wakati wa kampeni za Uchaguzi zinazoendelea katiika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, Kajuna amesema kuwa amekuwa ndani ya uongozi wa Simba kama Makamu wa Rais na amefanya mambo mengi sana na uamuzi wake wa kuwania nafasi ya Ukurugenzi wa bodi ni kumalizia alipoishia.

Amesema kuwa, mawazo yaliyopo katika Klabu ya Simba anahitaji kuyaendeleza na kufikia malengo ya  Kuwa na uwanja wake, kuwa na kituo cha kukuzia soka vijana pamoja na hosteli za timu.

"Nimekuwa makamu wa rais wa Simba kwa muda kidogo na tumefikia katika hatua nzuri ya kuelekea katika mabadiliko, naomba ridhaa ya wanachama nirejee kwenye Uongozi wa klabu ya Simba ili nikamalizie pale nilipoishia,"amesema Kajuna.

"Tumekuwa na mikutani mingi ya usiku na mingine ikimaizika saa nane usiku, yote ikiwa ni katika kuijenga Simba mpya, Simba ya mabadiliko ya kuingia kwneye mfumo wa hisa na tumefanikiwa katika hilo,"amesema

Kajuna amesema kuwa, mbali na hilo ataweka zaidi ukaribu na wanachama zaidi ya huu aliokuwa nao sasa hivi, ataweka maslahi mbele ya Klabu ya Simba pamoja na kuhakikisha Simba wanapata ushindi kwa hali yoyote ile.

Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya uchaguzi wake November 04 ukihusisha nafasi ya mwenyekiti wa klabu na wajumbe watano watakaoingia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi.

Kampeni za Uchaguzi zinaendelea kwa wagombea kunadi sera zao pamoja na mikakati walioiweka ili kuifikisha Simba kuwa moja ya timu Afrika ikiwemo kuchukua Klabu Bingwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad