HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 21 November 2018

WAJUMBE KAMATI YA MAREKEBISHO YA KATIBA, KAMATI YA WATAALAM CPA KANDA YA AFRIKA WAKUTANA KWA MAJADILIANO

 Mwenyekiti wa kamati ya marekebisho ya katiba kutoka Bunge la Ghana, Mhe. Osei  kyei Mensahu Bonsu (katikati) akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo, kamati ya wataalam katika kikao cha kamati maalum ya utendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA) kinachoendelea leo tarehe 21 Novemba 2018 Bahari Beach Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa kanda wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA), Ndg. Stephen kagaigai, kulia ni Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa kamati ya wataalum ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA), Ndg. Cecilia Mbewe.
 Wajumbe wa kamati ya marekebisho ya katiba kuanzia kushoto ni aliekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Nigeria na Mweka hazina wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA), Mhe. Samuel Ikon, Mwakilishi wa Kanda kutoka Bunge la Namibia Mhe. Bernard Sibalatani na kulia ni Mhe. Vedasingam Baloomoody Mbunge kutoka Bunge la Mauritius wakiwa katika kikao cha kamati maalum ya utendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA) kinachoendelea leo tarehe 21 Novemba 2018 Bahari Beach Jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa kamati ya wataalam na Mshauri wa masuala ya kisheria kutoka Bunge la Ghana, Ndg. Ebenezer Djietror akizungumza na wajumbe wa kamati ya marekebisho ya katiba, kamati ya wataalam katika kikao cha kamati maalum ya utendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA) kinachoendelea leo tarehe 21 Novemba 2018 Bahari Beach Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa kamati ya wataalam na mshauri wa masuala ya kisheria kutoka Bunge la Uganda, Ndg. Jacqueline Guma

 Wajumbe wa kamati ya marekebisho ya katiba, kamati ya wataalam wakiwa katika kikao cha kamati maalum ya utendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA) kinachoendelea leo tarehe 21 Novemba 2018 Bahari Beach Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad