HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 26, 2018

WADAU WA SEKTA YA AFYA KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA NCHINI


NA WAJMW-DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kuboresha huduma afya nchini kwa kukarabati vituo vya afya vipatavyo 350 ili  utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto hususani  huduma za dharura wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika mapema  jijini Dodoma.
“Sekta ya afya tunaona inaendelea kupiga hatua kubwa sana katika maeneo mbalimbali ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu ambapo vituo vya Afya takribani 350 vimekarabatiwa kwa  kuongeza miundombinu kwa ajili ya kutoa huduma za afya za dharura ikiwemo huduma za kumtoa mtoto tumboni”.
Waziri Ummy amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani inahakikisha sekta ya afya inapata mafanikio kwa kuboresha huduma nchini ikiwemo na kufikia asilimia zaidi ya 90 ya dawa zinapatikana katika sehemu zote za kutoa huduma.
Aidha, Waziri Ummy amesema mkutano huo ulikua na lengo la kukubaliana kutekeleza vipaumbele nane (8) ambavyo serikali pamoja na wadau wa maendeleo itahakikisha vinatekelezwa ipasavyo katika mwaka 2019/2020.
Maeneo hayo ni pamoja na Kuimarisha huduma za afya ya uzazi ,mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuweka miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura na watoto wachanga kwani kwa takribani hivi sasa watoto wachanga wapatao elfu tisini hufariki ndani ya siku ishirini na nane (28) za mwanzo. Kuongeza huduma za uzazi salama sambamba na uzazi wa mpango, kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka mama kwenda kwa mtoto.
Eneo la pili linahusu Afya za wasichana na wavulana walio katika umri wa kubalehe ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuepuka ngono katika umri mdogo na mimba zisizotarajiwa.
Alitaja eneo jingine  ni kuongeza nguvu kazi katika sekata ya afya ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi wa afya katika ngazi zote, kuongeza ujuzi kwa kutoa nafasi za kusomesha watumishi ili kukidhi vigezo vilivyoweka na shirika la afya duniani (WHO).
Kipaumbele cha Nne, ni kuimarisha ubora wa huduma za afya utakaoenda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya sehemu za kutolea huduma za afya za serikali pamoja na kuongeza rasilimali fedha kwa ajili ya kutatua changamoto za afya kwa kuongeza  ya bajeti ya afya   kutoka kutoka Bilioni 31 hadi Bilioni 270 mwaka 2018/2019.
Naye Naibu katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia afya dkt.Zainabu Chaula amesema kwamba wao kama sehemu ya utekelezaji wamejipanga kutekeleza maboresho ya afya ngazi ya msingi kuanzia vijijini hadi Taifa kupitia sera ya afya hivyo wamejipanga kuongeza kutoa elimu ya afya kwa umma kuanzia zahanati  kwa kupanga mipango endelevu ili iende sambamba kuanzia ngazi husika kwa kutumia kamati za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.  
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa maendeleo na wakurugenzi wa wizara (Hawapo Pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma.
 Wakurugenzi mbalimbali kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo Pichani) katika mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma
 Wadau mabalimbali wa maendeleo wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yanaendelea katika mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katikati) akisaini makubaliano ya malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020. Kushoto ni Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Kulia ni Mwakilishi wa wadau wa maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad