Na Geofrey Tengeneza
Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara Andrew Rosindell
ameahidi kusaidia kufanikisha mpango wa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kufanya
Safari zake London, Uingereza.
Rosindelli alitoa ahadi hiyo jana alipokutana na kuwa na mzungumzo na Naibu
Katibu Mkuu wa WIzara ya Maliasili na Utalii Dkt Aloyce Nzuki katika maonesho ya utalii ya
World Travel Market yanayoendelea jijini London Uingereza ambapo alimuomba mwakilishi
huyo kusaidia mpango huo ambao alisema utasaidia sana kuongeza idadi ya watalii
wanaotembelea Tanzania kutoka Uingereza.
Aidha Dkt.Nzuki amemuomba Rosindell kuandaa mkutano wa pamoja baina yawafanyabiashara wa Tanzania na Uingereza mapema iwezekanavyo ili kujadiliana namna ya
kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uingereza kwa
manufaa ya nchi hizo mbili.
Aidha, Dkt.Nzuki ameweza kukutana na kufanya mazungunzo na Mjumbe maalum ambaye pia
ni Mbunge wa nchi hiyo Andrew Rosindell ambaye ni mbunge aliteuliwa na Waziri Mkuu huyo
kuwa Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza wa masuala ya Biashara (Trade Envoy) ambaye
miongoni mwa kazi zake ni kukuza biashara, uwekezaji na Utalii baina ya Uingereza na
Tanzania.
Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt.Hamisi Kigwangalla
amepongeza timu ya Tanzania inayoshiriki maonyesho hayo kwa kazi nzuri ya kuitangaza
vyema Tanzania kama eneo bora la utalii Afrika na Duniani kwa ujumla.
Kupitia ukurasa wake Twitter aliandika "hii ni taswira ya leo ya banda letu la maonesho kule
ambapo timu ya washiriki kutoka Tanzania ikijumuisha waoneshaji kutoka sekta ya umma na
jijini London, kwenye World Travel Market (WTM), Uingereza, ambapo slogan yetu ya
Tanzania Unforgettable! imetumika ipasavyo kuuza vivutio vyetu. Nawapongeza sana washiriki
wote kutoka Tanzania na wa Kamati yetu ya Destination Branding chini ya uenyekiti wa
Devotha Mdachi kwa kazi nzuri. Huu ni mwanzo tu” aliandika DKt Kingwangala.
Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umeratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania –TTB
binafsi inaongozwa inaongozwa na Naibu Katibu MKuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.
Aloyce Nzuki.
Naibu Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Dkt.Aloyce Nzuki akimkabidhi majarida na vipeperushi vya utalii wa Tanzania (promotional materials) mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara Andrew Rosindell .
Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya biashara Andrew Rosindell akisoma moja ya majarida ya utalii alipotembelea banda la
Tanzannia katika maonesho ya World Travel Market jijini London Uingereza.
No comments:
Post a Comment