HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 24 November 2018

Taifa linahitaji watakwimu katika kusukuma maendeleo- Dkt. Kijaji

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kufikia uchumi wa kati kufikia 2025 kunategemea kuwepo kwa takwimu rasmi na bora  ambazo ndio zitaonesha maendeleo yaliyofikia kufika mwaka huo. Dkt Ashatu ameyasema hayo katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es salaam.

 Amesema kuwa wahitimu wa chuo cha takwimu wanajibu wa kufikiria ni kitu gani wanaenda  kuzalisha kwa taifa kuweza kunufaika na utalaam huo kwa maendeleo ya taifa. Dkt. Ashatu amesema kuwa kupungua idadi ya wanaojiunga katika chuo cha takwimu sio tatizo kwani wanaohitajika ni watu wenye ujuzi na ubunifu ambao wataleta mageuzi ya takwimu katika taifa.

Aidha amekiagiza Chuo hicho kufundisha takwimu shirikishi kutokana na kuwepo maswali mwngi yanayotoa changamoto kwa wananchi hivyo ni chuo kiweze kutatua changamoto hizo kupitia takwimu shirikishi. “Bila takwimu hakuna mipango na mipango bila takwimu hakuna maendeleo hivyo wahitimu lazima muonyeshe ujuzi na umahiri wenu katika ofisi mtazoenda kufanya kazi na kuleta mabadiliko  chanya  ya kusaidia taifa”amesema Kijaji.

Amesema kuwa chuo kinawajibu wa kuzalisha watalaam wenye weledi ambao watakidhi soko la ajira kutokana na eneo hilo kuwa muhimu katika maendeleo ya nchi yeyote duniani. Kaimu Mkuu wa Chuo Takwimu Dkt. Frank Mkumbo amesema kuwa safari haikuwa ndogo katika kufikia siku ya leo katika kuwaandaa watalaam ambao wataleta mbadiliko katika sekta ya takwimu.

Amesema kuwa wameanzisha shahada ya takwimu za kilimo kutokana na uhitaji wake mkubwa kwa taifa kupata takwimu rasmi katika sekta hiyo kwa kushirikiana na NBS pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi. Dkt Mkumbo amesema chuo hicho kinapata wanafunzi katika nchi mbalimbali za Afrika  baadhi ya nchi hizo  ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana, Zimbambwe , Elntrea , Sudani Kasikazi na Sudani Kusini, Ephiopia, Ghana, Msumbiji
 Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri wa Chuo hicho Dkt Albina Chuwa akiazungumza kuhusiana mahitaji ya watalaam watakwimu katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Takwimu  Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Dkt Frank Mkumbo akitoa taarifa ya Mahafali ya Nne ya Chuo Takiwimu Takwimu yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji akitunuku wahitimu katika chuo cha Takwimu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad