HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 19 November 2018

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAWAPA SOMO WABUNGE JUU YA WATOTO NJITI

KILA ifikapo Novemba 17, Dunia huadhimisha siku ya mtoto njiti (World Prematurity Day) na kwa umuhimu wake, Taasisi isiyo ya kiserikali ya Doris Mollel yenye jukumu la kuhakikisha Mtoto Njiti anapata mahitaji yote muhimu na kukua iliendesha semina kwa Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti).

Semina hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa wabunge wanawake Tanzania (TWPG) ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Katika semina hiyo, Taasisi ya Doris Mollel ilipendekeza ombi kwa Serikali la kurekebisha sheria ya likizo ya Uzazi ili wazazi wenye watoto njiti waweze kupata muda wa kutosha kulea watoto wao ambao asilimia kubwa huwa na changamoto nyingi pindi wazaliwapo, hivyo huhitaji uangalizi wa hali ya juu kutoka kwa wazazi wao.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu ya Saidia  wazazi wenye watoto njiti na watoto wagonjwa.

Pamoja na semina hiyo, Taasisi ya Doris Mollel pia imekabidhi vifaa tiba katika Hospitali ya wilaya ya Kongwa, Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na Hospitali kuu ya kambi ya wakimbizi, Nyarugusu ambayo itakabidhiwa wiki hii.

Shuguli za maadhimisho ya mtoto Njiti mwaka 2018 zimefanikishwa kwa Ushirikiano na Wizara ya Afya pamoja na wadau wengine wa maendeleo kama Vodacom Tanzania Foundation, Benki ya DTB, Benki ya CBA, Asas Dairies, Ashton Media,
Sign Express LTD n.k. 

Pichani ni Sehemu ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa pamoja na Ujumbe kutoka Taasisi ya Doris Mollel pamoja na washirika wengine katika semina hiyo.
Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe akitoa mada katika semima kwa Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo mbele ya Wangunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa semina iliyozungumzia umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma.
Sehemu ya Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifatilia mada hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad