HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 2 November 2018

Salomon Kalou adhihirisha Umri ni namba tu ligi ya Bundesliga

Wikiendi hii ni mzunguko mwingine wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga na miongoni mwa michezo ambayo itakuwa ya kuvutia sana ni ule wa RB Leipzig dhidi ya Hertha Berlin. Leipzig hawajashuka sana ukilinganisha na kiwango walichokuwa nacho msimu uliopita, Hertha Berlin pia wana msimu mzuri hadi sasa ikiwa ni tofauti tu ya magoli ndiyo inawatofautisha na Leipzig ambao wako nafasi ya tano kaatika msimamo wa ligi.
Hertha Berlin kwa sasa wanatamba na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Salomon Kalou ambaye amedhidi kudhihirish kuwa umri ni namba tu, wiki iliyopita alifunga mabao mawili katika droo dhidi ya vinara wa ligi hiyo Borussia Dortmund. Kalou anatarajiwa kuwa tishio tena katika mchezo huo wa wikendi hii.
Mchezo huu utakuwa moja kwa moja kupitia chaneli ya ST World Football ndani ya king’amuzi cha StarTimes tena kwa lugha ya Kiswahili, kuanzia saa 2: 30 Usiku jumamosi tar 3 Novemba.
Michezo mingine katika ligi ya Bundesliga wikiendi hii ni Bayern Munich vs Freiburg (LIVE kwenye ST World Football saa 11: 30 Jumamosi), Schalke vs Hannover, Bayern Leverkusen vs Hoffenheim, Wolfsburg vs Borussia Dortmund na siku ya Jumapili ni Borussia Monchengladbach vs Dusseldorf na Mainz vs Werder Bremen. Michezo yote itakuwa Mubashara kupitia chaneli za michezo za StarTimes.
Napo katika ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 wikendi hii michezo kadha wa kadha itapigwa katika viwanja vikubwa kwenye ligi hiyo, mabingwa Paris St Germain wanacheza usiku wa leo dhidi ya LOSC Lille saa 4:45 Usiku Mubashara kupitia ST World Football, PSG wanacheza katika kiwango bora kabisa kwa sasa huku wakijivunia nguvu kazi ya washambuliaji wao kama mbrazil Neymar, kinda wa Ufaransa Kylian Mbappe na fowadi wa Uruguay Edinson Cavani ambao ni tishio kwa safu yoyote ya mabeki kwa sasa.
Siku ya jumamosi michezo mingine itaendelea ambapo Lyon watacheza dhidi ya Bordeaux saa 1 jioni, Stade Reims dhidi ya AS Monaco na Jumapili ni Montpellier dhidi ya Olympic de Marseille, michezo hii itakuwa Mubashara kupitia chaneli za michezo za StarTimes.
Kwa wateja wanaotumia ving’amuzi vya Antenna mechi zote zitakuwa katika kifurushi cha MAMBO ambacho kinapatikana kwa Tsh 14,000/ tu na kwa watumiaji wa ving’amuzi vya Dish chaneli za michezo zinapatikana katika kifurushi cha SMART kwa Tsh 21,000/= tu. Kumbuka mechi za Bundesliga zinakujia kwa lugha ya Kiswahili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad