HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 30 November 2018

RC MAKONDA KUPAMBA SHEREHE ZA MIAKA 18 YA MAGIC FM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, anatarajiwa kuzipamba sherehe za kutimiza miaka 18 tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio cha Magic FM kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa vipindi na maudhui Orest Kawau amesema sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya shule ya Tandale hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi.

Pia amesema zawadi mbalimbali zitagawiwa kwa wasikilizaji wa kituo hicho cha Magic FM na kwa watakaowahi watajipatia zawadi maalum.

"Tumeamua kuadhimisha miaka 18 ya Magic FM ili kurudisha fadhila kwa wasikilizaji wetu ambao wametuunga mkono kwa kipindi chote tangu tulipoanza mpaka sasa. Tunawaomba watanzania waendelee kutuamini na tunaahidi kuwapa ladha inayostahili kwa wakati wote" Alisema Kawau.

Kwa upande wake Balozi wa Kampuni ya bahati nasibu ya Daka Pesa ambao ni wadhamini wakuu wa hafla hiyo Salum Salehe amesema kampuni imeamua kudhamini ili kuungana na kituo hicho hasa katika kutoa elimu juu ya huduma wanazotoa kupitia mchezo wao wa Daka Pesa  ambapo mteja anaweza kucheza kwa kiwango cha kuanzia 500 na kujishindia zaidi ya milioni 1.

Mkuu wa vipindi na Maudhui kutoka redio Magic Fm, Orest Kawau akizungumza kuhusiana na maadhimisho miaka 18 tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio cha Magic FM kesho yatakayofanyika kesho.
 
Balozi wa Daka Pesa, Salum Saleh (kulia) akizungumza jambo kuelekea maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa kituo cha Redio cha Magic FM kesho.
Balozi wa Daka Pesa ambao ndio  wadhamini wa sherehe hizo, Salum Saleh (kulia) akionysha bango  la kampuni yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad