HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 3 November 2018

PROF MKUMBO AONGOZA ZOEZI LA KUHAKIKI MITA ZA MAJI WA WATEJA WA DAWASA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akijaza fomu ya maji baada ya kusoma mita ya mteja wakati wa zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo akiwa ameambatana naMeneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson leo Jijini Dar es Salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ameendesha zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo.

Zoezi hilo liloandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) ni la siku moja lenye lengo la kuwezesha mamlaka kuwa na taarifa za wateja na kuhakiki usalama na ubora wa mita.

Usomaji na uhakiki wa mita hizo za wateja utakuwa ni kwa Mkoa wote wa Dar es salaam, Pwani ikiwemo Kibaha na Bagamoyo na litaendeshwa na wafanyakazi wa DAWASA.

Profesa Mkumbo amesema kuwa, zoezi hilo litamsaidia Mteja kufahamu kiasi cha maji anachotumia pia itapunguza upotevu wa maji na kupelekea hasara mamlaka.

Mbali na hilo, amesema kuwa zoezi hili litasaidia Mamlaka kupata njia za kudhibiti upotevu wa maji kama Waziri alivyowaagiza kuhakikisha wanapunguza na kushiriki kwake ni katika kuunga mkono jitihada za DAWASA 

Mkumbo amewapongeza DAWASA kwa kuweka mita nzuri na zingine zikiwa mpya kabisa na zinafanya kazi vizuri na hata wateja aliokutana nao wameonesha kupendezwa na huduma za mamlaka hiyo katika utoaji wa maji safi na salama.

Meneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson amesema kuwa zoezi hili limekuwa na tija kubwa sana na kwa mwenendo huu wanaweza kubaini wateja wanaotumia maji kwa wingi na hata wale wanaoiba maji na wameweza pia kuona mivujo na kuweza kuiziba.

Kwa upande wa Tanesco mhandisi Laura Hyera amesema kuwa DAWASA wanafanya jambo zuri sana kuja kusoma mita hizi mara kwa mara, inasaidia kumpa mteja au mtumiaji wa maji kujua kiasi anachokitumia.

Hyera amesema anawapongeza sana kwa hatua hiyo itajenga uaminifu kwa wateja wa DAWASA kulipa maji kwa wakati na kuzuia wizi wa maji.

Profesa Mkumbo ametembelea wateja wakubwa akiwemo Tanesco na kusoma mita mbili zilizopo pale na kuhakiki ubora wake, wateja wadogo wa eneo la Changanyikeni na kufurahishwa na utendaji kazi wa DAWASA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akijaza fomu ya maji baada ya kusoma mita ya mteja wakati wa zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo akiwa ameambatana naMeneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akisoma mita ya mteja wakati wa zoezi la kusoma na kuhakiki mita za maji kwa wateja wakubwa na wadogo akiwa ameambatana naMeneja wa DAWASA Ubungo Mponjoli Damson leo Jijini Dar es Salaam. No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad