HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 18 November 2018

POLISI PWANI YAMSAKA MWANAMKE ALIYEMPIGA MWANAE WA MIAKA MITANO HADI KUMSABABISHIA KIFO -NYIGESA


NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani ,linamtafuta mwanamke ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto  wake Halima Ramadhani (5) kwa tuhuma za kuunguza pazia la chumbani.

Kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa alithitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha huko Kikongo wilaya ya Kipolisi Mlandizi wilayani Kibaha

Alisema mama huyo ,  alimuua mwanaye kwa kipigo akimtuhumu mwanaye huyo kuunguza pazia hilo kwa kutumia kibatari.

"Baada ya kukuta pazia hilo limeungua mama yake alimshambulia na kupelekea kifo cha mtoto huyo na alipoona hali mbaya alikimbia," alisema Nyigesa.

Alisema,mtoto huyo alifariki alipofikishwa katika kituo cha Afya Mlandizi siku hiyo hiyo majira ya saa nne usiku.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad