HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 22, 2018

MTIBWA SUGAR KUTUMIA UWANJA WA AZAM COMPLEX MICHUANO YA SHIRIKISHO AFRIKA



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Klabu ya Mtibwa Suga ya Turiani Morogoro inayowakilisha Tanzanaia katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwa msimu wa 2018/2019 wanatarajia kutumia Uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani.

Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi November 27 na 28 mwezi huu Mtibwa Sugar wamepangiwa kucheza dhidi ya Nothern Dynamos ya Usheli sheli.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Norhen Dynamo ya Shelisheli.


"Tumebeba dhamana ya watanzania katika michuano hiyo kazi yetu kubwa ni kuweza kupata matokeo hilo ndilo jukumu ambalo nimewapa wachezaji wangu, wote wanalitambua hilo," alisema.

Mtibwa Sugar wanaingia kwenye michuano hiyo baada ya kukamilisha adhabu yao ambayo walipewa ya kutoa faini baada ya kushindwa kupeleka timu kwenye michuano hiyo nchini Afrika kusini kutokana na Ukata.


Wana tam tam wanatarajia kuanzia uwanja wa nyumbani katika kutupa karata yao ya ushiriki wao katika michuano hiyo na uongozi wa juu wa klabu hiyo kupitia kwa msemaji wao Thobias Kifaru tayari umethibisha kuwa watatumia uwanja wa Azam Complex,Chamazi katika michuano hiyo kwa michezo ya nyumbani.

“kila mmoja anajua tunatumia uwanja wa Manungu kama uwanja wetu wa nyumbani pia tunautumia uwanja wa Jamhuri kwa michezo miwili tu ya ligi kuu dhidi ya Simba na Yanga lakini katika michuano hii ya kimataifa tumeshindwa kutumia viwanja hivi viwili kutokana na viwanja vyote viwili kutokidhi hadhi ya kimataifa ya michuano hiyo hivyo tumeamua kuutumia uwanja wa Azam Complex uliopo Mbande ,Mbagala, hivyo tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi” Kifaru

Mtibwa Sugar wamepangiwa kucheza dhidi ya Nothern Dynamos ya Usheli sheli katika kombe la shirikisho na baada ya mchezo huo wa jijini Dar es saalaam wana tam tam watasafiri kuelekea Usheli sheli kwa ajili ya mchezo wa pili wa marudiano na mchezo wa marudiano utachezwa kati ya Desemba 4 au 5.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad