HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 27, 2018

MSANII AMBER RUTTY NA MPENZI WAKE WAACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA KUTIMIZA MASHARTI

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Baada ya kusota rumande kwa takribani siku 25, hatimaye leo Novemba 27, 2018 msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' na mpenzi wake Said Bakary wamefanikiwa kupata dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.

Amber Rutty amedhaminiwa na  Salma Omary Bungo (46), na
Asha Mohammed (46) huku anayedaiwa kuwa mpenzi wake akidhaminiwa na mchungaji Daud Mashimo pamoja na Francis Chacha.

Mahakama iliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini 2,  ambapo kila mmoja  amesaini bondi ya Shilingi Milioni 15 wakitakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria. Aidha mahakama imewaamuru wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Amber Rutty na Said Bakary walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na Amber Rutty na Said Bakary ambao walishindwa kudhaminiwa kwa mara tatu mfululizo mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Charles maarufu kama 'James Delicious' ambaye yeye alishadhaminiwa.

Wawili hao wameachiwa kwa dhamana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine Rwizire baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Katika kesi ya  kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, linalomkabili James Delicious imedaiwa Oktoba 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Katika kosa la kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Rutty na Said Aboubakary wanadaiwa Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp.
Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' akiwa anatoka katika maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti ya dhamana 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad