HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 8 November 2018

Msafiri:Viongozi wa umma kuzingatia sheria na kuyaishi maadili ya kazi katika kujiepusha na mgongano wa kimasilahi

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri amewaasa viongozi wa umma kuzingatia sheria na kuyaishi maadili ya kazi ili kudhibiti migongano ya kimaslahi katika maeneo yao ya kazi.

Msafiri  ameyasema hayo leo wakati wa mafunzo ya kujadili rasimu ya kanuni za sheria ya maadili ya viongozi wa umma  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, amesema kwamba maadili ni tunu ya Taifa hivyo isipozingatiwa viongozi hujikuta katika hatari ya kuingia katika mgongano wa maslahi kwa kujua au laa! na wakati mwingine wanaingia katika mgongano huwa na kujipatia fedha nyingi na kuonekana kutumia vizuri cheo chake.

"Ni bayana kuwa mgongano wa maslahi ni changamoto ya kimaadili ambayo isipodhibitiwa unaweza kusababisha  mmonoyoko  wa maadili  kutokana viongozi wa umma kujiingiza katika mgongano wa kimasilahi huo" amesema msafiri.

Amesma  kuwepo kwa maslahi binafsi kwa viongozi kunaathiri maamuzi na usimamizi wa shughuli za umma..

" Ni muhimu sote tukakumbuka kuwa suala la ujenzi wa utamaduni maadili na uwajibikaji siyo la mtu mmoja kwa muda mrefu jitihada za kujenga uadilifu na kupambana na rushwa zimekuwa zikilenga sekta ya umma haigawi na watumishi wa sekta ya umma pekee" amesema.

Msafiri wapo watu wanaoshawishi watumishi wa umma wapokee rushwa ,baadhi yao wanatoka katika sekta binafsi,niwajibu wa kila mmoja aliyeshiriki katika warsha ya leo kutambua nafasi aliyonayo katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inaondokana na mgongano wa maslahi na utovu wa maadili kwa kukataa kuwa mbia katika vitendo hivyo.

Kwa upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu  Harold Nsekela amesema kuwa mgongano wa maslahi ni tatizo linaloathiri maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Nsekela amesema nchi nyingi duniani zinakabiliwa na tatizo hilo na madhara yake yanatofautiana kati ya nchi moja na nyingine kutegemea na kiwango cha ukubwa wa tatizo na kwamba tatizo la mgongano wa maslahi ni miongoni mwa matatizo ya kimaadili yanayochelewesha maendeleo kwa wananchi.

" Nchi nyingi zimejiwekea mifuko ya kikatiba, kisheria, kiutawala na miongozo mbalimbali ya namna ya kuzuia mgongano wa maslahi, mifumo ya kuzuia mgongano ya maslahi inatamkwa chini ya sheria na Kanuni mbalimbali ikiwemo sheria ya maadili ya viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 (sura 398), hivyo kanuni hizi zitaimarisha zaidi mfumo wa kudhibiti wa mgongano wa maslahi.alisema Nsekela.

Naye diwani wa kata ya  kimbiji wilaya ya kigamboni Sanya Muhidin Bunaya amesema kwamba viongozi wa umma wamekuwa wakijisahau kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheri na maadili ya utumishi,hivyo majadiliano hayo ya rasimu ya kanuni za sheria ya maadili itasaidia kudhibiti mgongano ya kimaslahi inayojitokeza mara kwa mara.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kujadili rasimu ya kanuni za sheria ya maadili ya viongozi wa umma iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu  Harold Nsekela akitoa maelezo kuhusiana na utendaji wa sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiwa katika kujiepusha na mgongano wa kimasilahi katika kujadili rasimu ya kanuni za sheria ya maadili ya viongozi wa umma iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili wa wa Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo katika kujadili rasimu ya kanuni za sheria ya maadili ya viongozi wa umma iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Sekretarieti ya  Maadili ya Viongozi wa Umma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad