HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 13, 2018

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB AENDELEA NA ZIARA YA KUJITAMBULISHA KWA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI JIJIJI DODOMA

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) wakati akimkaribisha ofisini kwake, Jengo la LAPF, Jijini Dodoma leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay. Viongozi wa Benki ya CRDB wapo jijini Dodoma kwa lengo la kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wateja wa Benki hiyo, sambamba na kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wao mpya ayepokea kijiti kutoka kwa Mtangulizi wake Dkt. Charles Kimei ambaye amestaafu. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) alipokuwa akizungumzia mikakati mbalimbali ya Benki hiyo pamoja na kujitambulisha kwake, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Dodoma, Rehema Hamisi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo, alipokutana naye Ofisini kwake, Jengo la LAPF jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Benki ya CRDB.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Alhaj Eng. Mussa Iyombe (katikati) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, kwa mchango waliotoa kwa Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliaji Fedha cha TAMISEMI, wakati uongozi wa Benki hiyo ulipomtembelea Katibu Mkuu huyo ofisini kwake, Jijini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliaji Fedha cha TAMISEMI, Miriam Mbaga.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Alhaj Eng. Mussa Iyombe (kushoto) akifafanua jambo mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati wa kikao chao kilichofanyika ofisini kwake, jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza.
Kikao kikiendelea.
Wakimsikiliza.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakifatilia mazungumzo hayo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kulia) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na viongozi wa Benki ya CRDB, waliofika ofisini kwake leo jijini Dodoma kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo.
Picha ya pamoja.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad