HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 23 November 2018

MASHINDANO YA VIJANA KUOGELEA KUFANYIKA DESEMBA 8 NA 9 MWAKA

Na Mwandishi wetu

Mashindano ya kuogelea kwa wachezaji yoso yamepangwa kufanyika Desemba 8 na 9 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini, yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali nchini na ya kimataifa.

Inviolata amesema kuwa TSA kwa sasa inatafuta wadhamini wa kufanikisha mashindano hayo. Mwisho wa kuthibitisha ni Novemba 30.
“Mashindano haya ni ya kuibua na kuendeleza vipaji, na pia yameandaliwa kwa ajili ya kupima uwezo wa waogeleaji chipukizi ambao wameibuliwa katika mashindano yaliyopita, tunaomba wadhamini wajitokeze,” alisema Inviolata.

Amefafanua kuwa wanatafuta wadhamini kwa ajili ya kusaidia gharama za uendeshaji kwani siyo kazi rahisi mashindano hayo kufanyika bila sapoti kutoka nje.

Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

“Mashindano haya yatatoa fursa kwa waogeleaji ambao walishindwa kushindana katika mashindano ya wakubwa kutokana na kigezo cha umri, kwa vile TSA inatamnbua waogeleaji chipukizi, tumeamua kuandaa mashindano ambao yatawafanya waogeleaji wanaochipukia nao kujipima uwezo wao,”alisema.

Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12. Washindi wa jumla katika kila kundi atazawadiwa kikombe wakati washindi wa kila shindano watapata medali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad