HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 24 November 2018

Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Na Mwandishi Wetu
Serikali imeteua jumla ya magereza kumi nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli la kulitaka  Jeshi la Magereza litumie  rasilimali  watu  ya  wafungwa kuzalisha  mazao kwa ajili ya biashara na chakula badala ya serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo hilo katika Gereza la Kwamngumi wilayani Korogwe ,mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya kilimo nchini na akiweka wazi uwapo wa mpango maalumu wa kutathmini na kupima mpango mkakati huo kwa kila gereza.
Aliyataja magereza hayo kuwa ni Songwe (Mbeya), Kitai (Ruvuma), Ludewa (Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule (Kagera) ambayo yameteuliwa kulima mahindi, mengine ni Idete na Kiberege (Morogoro) yaliyoteuliwa kulima mpunga huku Kitete (Rukwa), Kitengule (Kagera) na Gereza la Arusha yakiteuliwa kulima maharagae
“Tunahitaji matumizi sahihi ya rasilimali watu na ardhi tuliyonayo katika magereza yetu itumike ipasavyo kwa shughuli za uzalishaji ili tuweze kutekeleza amri ya Mheshimiwa Rais, huku lengo la wizara kupitia jeshi la magereza ni kuweza kuwekekeza fedha kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi hilo na ikiwezekana hapo baadae tuweze kutafuta wateja watakaonunua mazao yatakayozalishwa katika mashamba hayo,” alisema Masauni
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, alisema wao kama uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa aguzo hilo huku akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo ili waweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa zaidi.
 Naibu Waziri  wa  Mambo ya Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad  Masauni, akiangalia  ubora  wa  tofali  linalotengenezwa  na  wafungwa  ikiwa  ni  mpango wa  uongozi  wa  gereza  la  Kwamngumi  kukabiliana  na  changamoto  ya  makazi kwa  askari, Kulia  ni  Mkuu  wa  Gereza  hilo,Christopher Mwenda, lililopo   Wilayani  Korogwe, mkoani  Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa nyumba iliyojengwa   na matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamngumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Kushoto  ni  Mkuu wa Gereza hilo, Christopher  Mwenda. 
 Naibu  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia  tofali  ambazo zimetengenezwa na wafungwa wa Gereza la Kwamngumi, ambazo hutumika kujengea nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli  la  kutaka  wafungwa  watumike  katika shughuli za uzalishaji na kilimo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti), na ujumbe alioongozana nao wakipita mbele ya nyumba  iliyojengwa kwa kutumia matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamgumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad