HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 6 November 2018

KOCHA MATTHEW McCOLLISTER JUSAKA VIPAJI VYA WACHEZAJI WADOGO WA KIKAPU KESHO JMK PARK


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Rais wa  Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) Phares Magesa amesema kuwa  Kocha wa Kikapu Matthew McCollister ataendesha mafunzo kwa vijana na kusaka vipaji. 

Mafunzo hayo yatakayoendeshwa  7 Novemba yataanza  saa 3 asubuhi  na kutakuwa na ufunguzi wa mafunzo ya vijana ya kikapu, yatakayoendeshwa na Kocha huyo Matthew McCollister ambaye ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Marekani.

Mafunzo hayo yatafanyika viwanja vya JMK Youth Park, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni tarehe 7 na 8, Novemba, 2018.

Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) linaomba vijana wote wanaopenda kushiriki katika mafunzo haya wafike JMK Park ili kufaidika na mafunzo hayo, ambapo pia Kocha huyo atachagua baadhi ya vijana wenye vipaji ambao watapatiwa nafasi ya kufanya mafunzo zaidi nchini Marekani.

Tayari Kocha huyo amefanya mafunzo kama haya Arusha tarehe 3 - 5 Novemba, 2018.

TBF inaishukuru Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kituo cha michezo cha JMK Youth Park na wadau wengine kwa kufanikisha mafunzo na ziara hii Kocha Matthew.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad