HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 8, 2018

KAMPUNI YA VISA WASHIRIKIANA NA HALOTEL KULETA MALIPO YA QR KWA WATUMIAJI WA HALOPESA.

*Wateja milioni 1 na wakala 40,000 kupata huduma ya malipo ya Visa kupitia Halopesa. 



Kampuni ya Teknolojia ya malipo ya kimataifa ya VISA imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini Tanzania.

Huduma hiyo itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Visa kwenye simu ili waweze kufanya malipo ya biashara kwa salama na kuweka na kutoa fedha kwa mawakala wa Visa.Mteja yoyote wa HaloPesa, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawana akaunti ya benki, wataweza kufaidika na huduma hii. 

Lengo la huduma hii ni kuunganisha Watanzania zaidi kwenye mfumo wa malipo ya kimataifa, kuleta huduma ya malipo ya Visa ya usalama na urahisi kwa watumiaji na wafanyabiashara.

"Tunafurahia ushirikiano huu na mojawapo wa kampuni maarufu ya simu ya Halotel, Ushirikiano wetu na Halotel utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanaya malipo ya QR kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji na wafanyabiashara zaidi ya 40,000. Pia itasaidia kuongeza ushirikishaji wa kifedha kwa watumiaji ambao sasa wataweza kufaidika na kushiriki katika mfumo wa eco Visa ", alisema Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Kevin Langley.

Halotel ni moja ya  kampuni ya simu inayokua kwa haraka zaidi nchini Tanzania ambayo ilianzishwa mwaka 2015. Ndani ya miaka 3, Halotel imepata wateja zaidi ya milioni 4 na ambao zaidi ya milioni 1 wanatumia huduma ya Halopesa. Pia kampuni inao wakala 40,000 kote nchini.

"Tunajivunia kushirikiana na Visa katika mpango huu. Kwa ushirikiano huu, tutaweza kuwa na uwezo wa kuletea wateja wetu huduma za kimataifa za malipo za Visa na kuwawezesha wateja wetu kulipia na kulipwa kwa urahisi zaidi. "Alisema Naibu Mkurugenzi wa Halotel Nguyen Van Son.

Kupitia ushirikiano, HaloPesa itawapa watumiaji fursa ya kufanya malipo kutumia code ya QR ya Visa hapa Tanzania na kote duniani.

Visa kwenye simu huwawezesha watumiaji kupata fedha zao moja kwa moja kutoka kwa akaunti zao za benki kupitia programu zao za benki za simu za kulipa wafanyabiashara, kutuma fedha kwa watu binafsi bila malipo, pamoja na kuhifadhi, au kutoa fedha kwa wakala wote wa Visa.

Wafanyabiashara waliojiandikisha watapata msimbo wa kipekee wa QR na Nambari ya biashara ambayo wateja wanaweza soma kwa kutumia simu ya android au smartphone na kwa watumiaji wa simu ambazo sio android, watatumia namba ya USSD kufanya malipo. Fedha zinahamia moja kwa moja kutoka kwa akaunti ya benki ya mteja na kuenda kwenye akaunti ya mfanyabiashara na hutoa taarifa ya muda halisi kwa pande zote mbili.

Wakala wa benki waliojiandikisha pia watapokea msimbo wa QR na Nambari ya Nyongeza ambazo watumiaji wanaweza kusoma kwa kutumia simu ya android au smartphone na kwa watumiaji wa simu ambazo sio android, watatumia namba ya USSD ili kuweka au kutoa fedha kwa akaunti za benki zilizowezeshwa.

Kampuni ys Visa imejitolea kuimarsha na kupanua soko la malipo ya simu kote duniani na ushirikiana huu ni mojawapo ya mipango ya Visa katika kutelekeza hili.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad