HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 12, 2018

KAMANDA WA POLISI NJOMBE ALIA NA WANAOTUPA VICHANGA

 Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kupitia Mtandao wa Wanawake  umechukizwa na kulaani Vikali  vitendo vya akina mama kutupa watoto mara baada ya jeshi hilo nyakati za usiku  kumuokota  mtoto mwenye umri wa  takribani wiki mbili katika Dampo la Kipagamo mjini  Makambako akiwa mtupu.
 Tukio hilo limetokea Novemba 02,  mwaka auu Ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya kipolisi Makambako wakati likiwa kwenye doria ndipo lilipomuona mtoto huyo akiwa hai na kulazimika kumuokota kwa kushirikiana na Ustawi wa Jamii na kisha kumpeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tumaini Ilunda Wilayani Njombe.
 "Askari wakiwa kwenye doria walipomsikia mototo analia wakaenda kwenye jalala na kumkuta mototo huyu akiwa katika uchi wa mnyama, tunawaomba sana hasa wakina mama ni vema kama hata umeshindwa kabisa kutunza mtoto ukamleta katika vituo hivi ukamuweka pale nje masista kama hawa wangemuona na kumchukua kuliko vitendo kama hivi vya kinyama" alisema kamanda Mzinga
Katika hatua nyingine Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe ikiwa ni muendelezo wa siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi Mkoa Renatha Mzinga wametumia nafasi yao kama jeshi la polisi akina mama kutembelea katika kituo cha kulea watoto yatima cha Tumaini kilichopo Ikelu na kuonana na watoto pamoja na kutoa Misaada mbalimbali kama vile sabuni, sukari, pipi, unga na vitu vingine mbalimbali  vyenye thamani ya shilingi Laki Nne.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad