HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 22, 2018

JWTZ YAPOTEZA WENGINE WATATU DRC, AFRIKA YA KATI

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama mnavyofahamu linashiriki Ulinzi wa Amani ndani na nje ya Bara la Afrika.

JWTZ linasikitika kuwataarifu kwamba limewapoteza wapiganaji wake watatu (3) waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.           

Mashujaa wetu waliouwawa ni Koplo Mohamed Mussa, Koplo Erick Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya.  Miili ya marehemu hao tayari imepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuhifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Heshima za mwisho kwa mashujaa wetu hao zitatolewa katika sehemu ya kuagia Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kesho tarehe 23 Novemba 2018 kuanzia saa 2.30 asubuhi.  Vyombo vya Habari na Wananchi wanakaribishwa tuungane katika kuaga mashujaa wetu.

Mungu azilaze Roho za Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad