HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 26, 2018

Elimu zaidi inahitajika mapambano dhidi ya Ukimwi

 Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Bw. Peter Masika (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (kushoto) wakati wakisubiri kuanza kwa matembezi ya hisani ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) katika wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (mwenye miwani ya jua) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Bw. Peter Masika wakishiriki matembezi ya hisani ya 5 Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) wakati wa wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.

 Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wadau wa sekta binafsi akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko wakishiriki matembezi ya hisani ya 5 Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) wakati wa wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari mkoani Dodoma wakishiriki matembezi ya hisani ya 5 Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) wakati wa wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri (katikati) akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ambaye pia ni Mbunge wa Biharamulo, Mhe. Oscar Mukasa (kushoto).
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5Km ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko akizungumza kuhusu maandalizi pamoja na kuhamasisha uchangiaji wa hiyari unaohusisha mtu binafsi, taasisi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na makampuni kupitia 0684909090 wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko akifurahi jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye  wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (kulia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri akipeana mkono na Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Issa Ng’imba baada ya kuwasilisha mchango wa wizara hiyo wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Bw. Peter Masika akitoa ushauri wa jinsi TATU MZUKA pamoja BIKO wanavyoweza kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) ikiwa ni zoezi endelevu kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga.
 Mkali wa Danadana, Bi Hadhala  Charles almaarufu kama Ronaldo wa Bongo akionyesha umahiri wake wa kucheza na mpira wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
   Baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za serikali, wananchi pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari Dodoma walioshiriki matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki kuchangia fedha Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) wakati wa matembezi ya hisani ya 5KM kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa NACOPHA wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na sektretarieti wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja wakati wa hafla ya matembezi ya hisani ya 5KM kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwenye wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi yanayoendelea kutimua vumbi mjini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu
Elimu zaidi na kampeni inahitajika kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya Ukimwi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati akizungumza katika wiki ya maadhimisho ya juma kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani iliyoambatana na matembezi ya hisani na mauzo ya tisheti kwa ajili ya kuchangia mfuko wa mapambano dhidi ya Ukimwi.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alisema ipo mikoa takwimu za maambukizi mapya zinapanda huku maeneo mengine hali ikibaki kuwa vile vile.
Aliwataka wananchi kubadili tabia hasa kujitokeza kupima kujua afya zao ili kama wameathirika basi waanze kutumia dawa.
Shekimweri alisema juhudi za makusudi zinatakiwa kuhakikisha mapambano dhidi ya maradhi hayo yanaongezeka .
Alisema mkoa wa Dodoma, mathalani kwa sasa maambukizi mapya yamefikia asilimia 5 yakipanda kwa asilia mbili zaidi ya ilivyokuwa miaka 2011/12.
Lakini alisema maeneo kama ya Zanzibar maambukizi yamepungua na kusema ipo haja ya kutafiti na kueneza majibu ya utafiti kwa umma ili uweze kujihami na maambukizi mapya.
Alisema watu kama Zanzibar inaonekana wamefanya vyema kutokana na kuwa na taratibu njema za kuzuia ‘ngono’ zembe ikiwa na pamoja na matumizi mazuri ya nyumba za kulala wageni.
Pamoja na kuhimiza elimu na utafiti kuzuia maambukizi mapya alizungumzia haja ya kushawishi wadau zaidi kuchangia mfuko wa Ukimwi ambapo kilomita 5 za matembezi ya hisani zimechangia sh 14,500.000 kwa mauzo ya fulana na ahadi mbalimbali.
Alisema ipo haja ya kuandaa mkakati mpya wa kuwezesha kutunisha mfuko huo wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi ambao unahitaji zaidi ya shilingi bilioni tatu. Mkakati huo ni pamoja na kufanya harambee na kutengeneza bidhaa za mauzo kwa ajili ya mfuko.
Aliongeza kuwa mtu binafsi, taasisi au makampuni ambao wangependa kushiriki zoezi hili endelevu la kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi (ATF) wanaweza kutuma michango yao kupitia namba za 0684909090.
Matembezi ya hisani ya kilomita 5 ya uchangiaji wa mfuko wa kudhibiti Ukimwi Tanzania. Jumla ya fedha zilizopatikana ni kupitia mauzo ya tisheti na ahadi ni sh 14,450,000 kwenye matembezi ya hisani ya kuchangia ‘AIDS Trust Fund’ -Mfuko waUdhamini wa Kudhibiti Ukimwi. 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko alisema utafiti huo umebainisha kwamba kuna ongezeko na kunahitajika kufanyika marejeo ya mkakati wa kupambana na Ukimwi.
Aidha Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk Leo Zekeng  amepongeza hatua za serikali kukabiliana na ugonjwa huo ikiwamo kuchagiza wanaume kujitambua kwa kupima na kuwa na mipango mahususi ya kuzuia maambukizi kwa vijana.
Alisema baada ya miaka 30 ya mapambano dhidi ya Ukimwi bado dunia inashuhudia ongezeko la maambukizi mapya hususani kwa vijana na kusema ipo haja ya kutathmini mapambano na kuyajenga upya.
Alisema kwa mwaka kulikuwa na maambukizi mapya bilioni 1.8 duniani na kusema kuwa wengi wa walioambukizwa walikuwa vijana. Alisema anaamini ufahamu ukiwaingia watu wakapima na kujitambua wataweza kusaidia kumaliza shida iliyopo sasa.
Alisema mpango wa serikali wa kuchagiza wanaume kupima kujitambua na kupata matibabu kama wameambukizwa ni sehemu njema ya kampeni hiyo dhidi ya maambukizi mapya.
Alisema tukio la maadhimisho hayo ni muhimu sana katika kukumbushana umuhimu wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo na maambukizi mapya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad