Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa wadau wa Wizara hiyo katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Uzalendo na Utaifa iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam .
Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akiongea jambo na wadau wa Wizara hiyo (Hawapo katika picha) katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao ndio Wadhamini Wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Disemba 2018 Jijini Dodoma, akieleza jambo kwa wadau wenzake waliofika kuunga mkono uzinduzi wa kampeni hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi(kulia) akimvalisha nembo inayoashiria uzalendo Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao ndio wadhamini wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Disemba jijini Dodoma.
Wadau wa Sanaa kutoka katika sekta binafsi taasisi za Serikali wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment