HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 4, 2018

DAWASA YAENDESHA MSAKO WA WEZI WA MAJI JIJINI DAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)  wameendesha zoezi la msako wa kuwakamata wezi wa maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Zoezi hilo linaloendelea kwa kasi limefanikisha kukamatwa kwa  mkazi mmoja wa Mbezi Kati aliyetambulika kwa jina la Alhaji Londa ambaye anatuhumiwa kujiunganishia maji  na kuyauza kwa wenye magari ya kubeba maji usiku. 

Akishiriki katika zoezi la Kuwasaka wezi hao, Meneja wa Mkoa kazi DAWASA Kawe, Gilbert Massawe ameweza kufanikisha kukamatwa kwa mwizi huyo anayedaiwa kujiunganishia maji zaidi ya mwaka mmoja.

Katika kumbukumbu za kiofisi zinaonyesha kuwa Londa alikuwa anadaiwa Tsh. Milioni 1.8 na alisitishiwa huduma tangu mwaka jana  hata hivyo alijiunganishia maji kinyemela na kuanza biashara ya kuuza maji usiku. 

Gilbert amemtaka Londa Kujisalimisha kituo cha polisi na kueleza kuwa hatua kali zitachuku dhidi yake.

Baada ya DAWASA kufanya uchunguzi na kujiridhisha jana ili vamia nyumbani kwa mtuhumiwa na kukuta kweli alijiunganishia maji kama inavyoonekana pichani. 

Hatua za kisheria zimechukuliwa kwa majibu wa sheria ya DAWASA na kwa kosa hili  mtuhumiwa atashitakiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo  wizi wa maji, uharibifu wa miundombinu  ya maji na uhujumu  uchumi.
Meneja wa Mkoa kazi wa DAWASA Kawe Gilbert  Massawe (kulia) akishiriki katika operesheni ya kumkamatamkazi mmoja wa Mbezi Kati aliyetambulika kwa jina la Alhaji Londa ambaye anatuhumiwa kujiunganishia maji  na kuyauza kwa wenye magari ya kubeba maji usiku. 





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad