Na Grace Semfuko-MAELEZO
Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi
wa Miradi inayofanywa na Serikali ya
Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea
kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi
Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la
Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Darala la Nyerere
Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway
Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika
April 2016.
Daraja hilo linalovuka mkondo wa
maji wa Kurasini hadi Kigamboni Jijini
Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni
daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John
Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima
ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Ujenzi wa Daraja la Nyerere
ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo
katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni
kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.
Akizungumza katika ziara hiyo
Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema
ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa
Tanzania.
“Nimefurahishwa na ujenzi wa
Daraja hili uliojengwa na Kampuni ya CRJE ya wachina,wamefanya kazi nzuri, kwa
Tanzania daraja hili ni fursa za kiuchumi kwani litarahisisha usafirishaji na
kuepukana na vikwazo vilivyokuwepo awali kabla ya dara hili” alisema Cai Defang
Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
hifadhi ya jamii la NSSF Bw. William Erio amesema kukamilika kwa daraja hilo
kumekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwani limekuwa likiingizia Serikali
mapato yatokanayo na kuvusha magari fedha ambazo zimekuwa zikienda kufanya
shughuli zinazoinufaisha jamii ya kitanzania.
“Tunashukuru Serikali kuendelea
kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inasaidia jamii kwa asilimia mia
moja,mfano daraja hili ni moja ya vyanzo vya kiuchumi kwani fedha za makusanyo
hapa zinasaidia kuongeza kasi ya kuhudumia jamii kupitia ujenzi wa miradi
mingine” alisema William Erio wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge
la Jamhuri ya watu wa China alipotembelea kwenye mradi huo wa daraja.
Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang na watendaji wa (NSSF) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (wa katika) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wakitembelea daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam .(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la (NSSF) Bw. William Erio alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Daraja kwa sasa
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment