Na Agness Francis, blogu ya Jamii
BARAZA la sana Taifa (BASATA) limeufungia rasmi leo Novemba 12 mwaka huu wimbo Ujulikanao kwa jina la Mwanza ulioimbwa na msanii wa lebo ya Wasafi Raymond Mwakyusa, maarufu Kama Rayvanny.
Ambapo wimbo huo wa Mwanza alimshirikisha msanii mwenzake Naseeb Abdul (Diamond Platinumz).
Amesema hayo Katibu wa baraza la sana Taifa Geofrey Mngereza kuwa baraza limeamua kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji wa maadili ya kitanzania kwa msanii Rayvanny kutumia maneno yanayohasisha ngono katika wimbo huo.
Mgereza amesema pamoja na kuufungia wimbo huo baraza linawaonya wasanii hao, vyombo vya habari ama mtu yoyote kutoutumia kucheza au kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile.
"Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria la Baraza namba 23 ya mwaka 1984 na kanuni zake limepewa mamlaka ya kusimamia Sanaa, wasanii na mtu yoyote anayejishughulisha na kazi za sana hapa Nchini"amesema Mngereza.
Katibu huyo amesema kuwa Baraza hilo linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny,Diamond pamoja na Uongozi wa Wasafi Limited na kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuunda kazi za sanaa.
"Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi, sambamba na onyo hili pia Baraza linawakumbusha wasanii chini ya Wasafi kutoutumia wimbo huo na nyimbo zingine zilizofungiwa kwa namna yoyote ile "amesema katibu Mngereza.
Vile vile Baraza hilo limewataka WCB kuondoa wimbo huo mara moja kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kufika saa kumi kamili jioni ya Leo.
No comments:
Post a Comment