HABARI MPYA

Home Top Ad



Post Top Ad

Sunday, 11 November 2018

BARAZA LA WADHAMINI YANGA LATOA TAMKO NAFASI YA MANJI HAIJAZWI

Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Yanga George Mkuchika akionesha barua aliyojibiwa na Yusuf Manji.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Baraza la Wadhamini wa Yanga limetoa msimamo wake wa kumtambua Yusuf Manji kama Mwenyekiti wa Klabu hiyo.

Uamuzi huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mkuchika akionesha barua aliyojibiwa na Manji baada ya kurejea kwake Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Jioni hii katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, George Mkuchika amesema kuwa baada ya mkutano mkuu wa Yanga uliohudhuriwa na wanachama takribani 4500 uliamua kwa pamoja kukataa kujivua uongozi kww Yusuf Manji.

Mkuchika amesema kuwa, baada ya uamuzi huo wa wanachama waliamua kumuandikia barua Manji na aliwajibu hawezi kukataa maamuzi ya wanachama ila atarejea kuanza kazi rasmi Januari 15 2019.


Amesema kuwa, katika barua yake aliyojibiwa Manji aliandika kuwa kutokana na ushauri wa daktari uliomtaka akae nje mpaka Desemba 15 kwa ajili ya matibabu ameomba kuanza majukumu rasmi ya kuitumikia klabu hiyo Mwakani.

"Ni kweli mimi nilimuandikia barua Yusuf Manji baada ya maamuzi ya wanachama katika Mkutano Mkuu ya kutokubali kujiuzulu kwake na akanijibu mimi Mkuchika kuwa hawezi kupingana na maamuzi ya wanachama ww Yanga ila ameomba kwanza amalizie tiba kama alivyoelekezwa na daktari kuwa kufikia Desemba 15  atakuwa ameshamaliza matibabu na kazi rasmi ataanza Januari 15, 2019,"amesema Mkuchika.

Akiongelea suala la uchaguzi wa Yanga na nafasi zinazotakiwa kujazwa, Mkuchika amesema kwakuwa Mwenyekiti bado yupo hivyo nafasi yake haitajazwa na amewaomba kamati ya utendaji ya Yanga kuwasilisha barua hiyo kwa TFF ili kuwapa uthibitisho.

"Sisi kama Baraza la wadhamini tunafurahi sana kuona Yanga inafanya uchaguzi tena ni jambo la faraja kwani taasisi kama Yanga haiwezi kuendeshwa bila ya kuwa na uongozi, ila tumesikia kuwa TFF wameamua kutaka kusimamia uchaguzi huu kupitia kamati yao jambo ambalo linavunja katiba ya Yanga, " amesema Mkuchika.

Amesema kuwa, katiba ya Yanga inaruhusu kamati tendaji iliyopo kuchagua kamati ya uchaguzi na inaelekeza hivyo kwahiyo TFF kuchagua kamati yake na kwenda kinyume na maagizo ya Baraza la Michezo Taifa (BMT) sio sahihi, wanachofahamu BMT waliagiza TFF wakae meza moja na Yanga wajadiliane.

Kutokana na hilo Baraza limetoa ushauri kwa kamati ya utendaji wa Yanga kukaa meza moja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kujadili uchaguzi wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad