Waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Hussein Mwinyi ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miradi mitatu ya ujenzi wa Ofisi ya Bunge inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji la Jeshi hilo (SUMA JKT).
Mhe. Mwinyi alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kukagua miradi hiyo akiwa ameambatana na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Kanali Rajab Mabele.
“Nimeridhishwa hatua ya utekelezaji wa miradi mitatu inayotekelezwa na SUMA JKT ya ujenzi na ukarabati wa Ofisi ya Bunge, naishukuru Ofisi ya Bunge kwa kuliamini shirika la SUMA kwa ajili ya kutelekeza miradi hii,” alisema.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai alilipongeza SUMA JKT kwa kuendelea kutelekeza miradi hiyo kwa ufanisi na kwamba hadi sasa miradi yote inaendelea vizuri.
Alitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Bunge, ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa lift na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge.
Alisema kwa upande wa ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Bunge pamoja na ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Bunge tayari SUMA JKT wameshalipwa asilimia 40 na kazi zinaendelea vizuri.
“SUMA JKT ni shirika ambalo tumekuwa tukifanya nalo kazi na tunaridhika na kazi zao tunatamani wapewe miradi mingi ya Serikali,” alisema.



Katibu
wa Bunge Stephen Kagaigai akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi alipomtembelea ofisini
kwake leo mjini Dodoma. Waziri mwinyi ametembelea Ofisi ya Bunge kukagua
miradi mitatu 3 ya ujenzi ya inayotekelezwa na Suma JKT.

Katibu
wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi
Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya
hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia.
Nyuma ya Waziri Mwinyi (mwenye miwani ) ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT
Kanali Rajab Mabere na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT
Meja Jenerari Martin Busungu .

Katibu
wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa
SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge
wakati viongozi hao walipotembelea eneo linapojengwa lift katika Jengo
la Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma .

Katibu
wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi
Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya
hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia.
No comments:
Post a Comment