HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 10, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Maonesho ya kimataifa ya Utalii ya  Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14.

Maonesho hayo yameandaliwa na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) yatafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC yakiwa na lengo la kuwaunganisha wafanyabishara wadogo na wa kati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabishara kutoka masoko makuu ya utalii duniani yameweza kudhaminiwa na wadhamini kadhaa wakiongozwa na Tanzania Ocean Cruisng and Safaris Ltd.

Akizungumzia maandalizi kueleka maonesho ya mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa maandalizi yamekaamilika kwa asilimia kubwa na mgeni rasmi akitaraiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema kuwa, maonesho hayo yatakuwa yanafunguliwa kuanzia saa nne asubuhi nna kufungwa saa 12 jioni na huduma mbalimbali zitakuwa zinafanyika ikiwemo bidhaa za utalii, semina zitakazokuwa zinaendelea ambapo jumla ya mada 24 zitawasilishwa na watalaamu waliobobea kwenye masuala ya utalii.

Devotha amesema kuwa,maonesho  yatajumuisha jumla ya mataifa  27 kutoka nje ya Afrika na mataifa 15 ya ndani ya Afrika  na zote zitaleta bidhaa zao za utalii na pia kuhudhuriwa na vyombo vya habari 300 duniani.

"Maonesho haya yatahudhuriwa na mataifa 42, mataifa 15 yakiwa ni kutoka Afrika kama vile Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Congo, Malawi, Namibia, Zimbabwe, Ghana, Cote D'ivoire, Nigeria, Malawi, Tunisia, Misri na Afrika Kusini huku mataifa mengie 27 kutoka  nje ya Afrika nayo yatashiriki  wakiwemo Marekani, Canada, Sweden, Italy, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Ubelgiji, Australia, India na nchi zingine"amesema Devotha.

 Amesema kuwa  katika maonesho hayo pia kutakuwa na vyakula vya kiasili vitakavyopikwa hapo hapo na wanafunzi  kutoka vyuo vya utalii nchini
ili washiriki na wageni wawezse kufahamu vyakula vya kiutamaduni nchini.

Kwa upande wa Mdhamini wa maonesho hayo Tanzania Ocean Cruisng and Safaris Ltd, Meneja Mauzo na Masoko Christine Jengo amesema kuwa wamefurahi sana kuwa moja ya wadhamini wa maonesho hayo ambapo mikakati yao ni kuona wanazidi kuwekeza kwenye sekta ya utalii wa ndani ikiwemo wameongeza boti mpya za kisasa.

Washiriki wa maonesho hayo kutoka nchi mbalimbali duniani wamepata punguzo la bei la asilimia 20 kutoka kwa wadhamini mwenza wa maonesho hayo Ethiopia Airlines.

Baadhi ya mafunzo mengine yatakayotolewa kwenye maonesho hayo ni pamoja na kuwapeleka washiriki hao kutembelea kwenye hifadhi za Mkoani Arusha kama Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za Serengeti, huku kwa mkoa wa Iringa wakitembelea utalii wa kilimo na ardhi yoeru ya Mufindi pamoja na vivutio vingine vya kiutamaduni na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Katika maeneo mengine ni Tanga, Mafia ambapo watatembelea utalii wa bahari kivuko kikuu Papa Potwe(Whale Shark), Morogoro  kwenye milima ya Udzungwa na Hifadhi ya TAifa ya Mikumi pamoja na  Zanzibar.

Maonesho hayo yatazidi kuboresha katika sekta ya utalii ambapo lengo kuu ikiwa ni kuongeza watalii kutoka  nje ya nchi na ndani ya nchi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akizungumza na waandishi wa habari maandalizi ya kuelekea maonesho ya kimataifa ya Utalii ya  Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14. Kulia ni Meneja Mauzo na Masoko  wa Tanzania Ocean Cruising Safaris Christine Jengo na kushoto ni Meneja wa Ukumbi wa Kimataifa wa JNICC Assah Mwambene.
 Maandalizi ya mabanda ya maonesho ya Maonesho ya kimataifa ya Utalii ya  Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14  kwenye ukumbi wa kimataifa wa JNICC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad