HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 8 October 2018

WAZIRI KANGI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE

Na Felix Mwagara, Mwanza.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefiwa na mdogo wake aitwae Josiah Chitage Lugola, aliyekua anaishi jijini Mwanza.

Waziri Lugola ambaye ndiye Msemaji wa familia hiyo, alisema mdogo wake Josiah (51) alifariki dunia leo asubuhi Oktoba 7, 2018 na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Sekour Toure, jijini Mwanza.

Waziri Lugola aliongeza kuwa, msiba upo Kijiji cha Nyamitwebili, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoa wa Mara. 

Waziri Lugola alikua wilayani Bunda kikazi ndipo akapata taarifa hizo za kushtukiza za msiba wa mdogo wake.

Hata hivyo, Lugola alisema msiba huo ni wa ghafla, umeshtua familia na hakika mdogo wake huyo ameacha pengo kubwa katika ukoo wao. 

"Msiba huu ni mkubwa, na pia umetikisa familia yetu, kifo kinapangwa na Mungu, hivyo tunamuombea Mungu, mdogo wangu apokelewe peponi, amina," alisema Waziri Lugola.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, ametoa pole kwa Waziri Lugola pamoja na familia kwa ujumla.

"Wizara inatoa pole kwa familia ya Waziri Lugola, ndugu wote, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo," alisema Kingu.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, taarifa za mazishi zitatolewa baada ya kikao cha familia.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad