HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 11, 2018

WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA

 Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye jengo la utawala la shule ya sekondari Kawawa wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
  Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawawa iliyopo Mafinga Mkoani Iringa.
  Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
Na hili ndio jengo la kisasa la utawala la shule ya sekondari ya kawawa lililofunguliwa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


WAZIRI wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari ya Kawawa kwa ujenzi wa jengo la kisasa la utawala ambalo litachangia katika ufanisi bora wa kazi kwa walimu na wafanyakazi wote wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa kuzindua jingo hilo la utawala waziri Mwinyi alisema kuwa jingo limejengwa kwa viwango ambavyo serikali ya awamu ya tano inataka na jingo hilo linaviwango vinavyotakiwa.

“Kwa kweli nisiwe mchoyo wa fadhila jingo hili limejengwa kwa kuzingatia ujenzi unaotakiwa na lina ramani ambayo itadumu kwa miaka mingi na itakuwa auheni kwa wafanyakazi kufanya kazi zao kwenye jingo hili” alisema Mwinyi

Waziri Mwinyi aliwataka wafanyakzi wa shule hiyo kuhakikisha wanalitunza jingo hilo pamoja na miundo mbinu yake kwa ajili ya vizazi vingine.

Awali akisoma risala kwa waziri Mwingi mkuu wa shule hiyo Meja Generali Erenest Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la utawala limejengwa kwa shilingi 222,591,000 na kufanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 103,360,000 kwa kuwa hapo awali BOQ ilikuwa inaonyesha kuwa gharama za jengo ni shilingi 325,951,000.

Kupungua kwa gharama hizo ni kutokana na ubunifu,matumizi mazuri ya rasilimali,nidhamu katika matumizi ya fedha,nguvu kazi ya vijana ambao baadhi yao walikuwa mafundi na gari kubwa la kusombea mchanga,kifusi na mawe msaada huo ulitoka katika kikosi cha 841kj Mafinga” alisema Maj  Sikaponda

Maj Sikaponda aliwashukuru wadau mbalimbali ambao walitoa msaada wa hali na mali kusaidia ujenzi wa jengo hilo la kisasa la utawala ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa shule hiyo.

“Mheshimiwa waziri tunapenda kuwashukuru wadau wafuata TANROAD mkoa wa Iringa kwa msaada wa kifusi cha kujaza msingi kwa trip mia,kampuni ya kichina inayojenga barabara ya Mafinga Igawa kwa msaada wa tripu moja ya kokoto ya ujazo wa Mita 15 za mraba,Clement Sangale saruji mifuko 20, na Beruto Kaboda alitoa mbao 2x3 Arobain” alisema Maj Sikaponda

Aidha Maj Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la kisasa la utawala linakabili na changamoto ya ukosefu wa samani kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo walimuomba waziri kuwasaidia kuzipata samani hizo.

Tumalizie kwa kumshukuru mkuu wa majeshi ya JKT Tanzania pamoja na bodi ya shule kwa usimamizi mzuri wa mipango ya maendeleo ya shule hii.

Kwa upande wake mkuu wa majeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu aliwapongeza viongozi waliosimamia ujenzi wa jengo hilo hadi lilipofikia na kuhakikisha linajengwa kwenye ubora unaotakiwa.

Maj Gen SM Busungu alimuomba waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa DR Mwinyi kwenda kuwaombea samani TRA ambazo walizitaifisha kutoka bandarini ambazo maarufu kama samani za makonda ili ziweze kutatua changamoto hiyo katika jengo hilo la utawala.

Akijibu ombi hilo la mkuu wa majeshi ya JKT waziri Mwinyi alisema ataenda kuwaomba TRA kwa kuwa wote wanaitumikia serikali moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad