HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 8, 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUENZI VITU VYA KIASILI KUVUTIA WATALII

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Watanzania wameombwa kuenzi vitu vya asili ili kudumisha utamaduni na kuvutia watalii wengi kuja nchini.



Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga alipokua anazungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Nchini baada ya kuwatembelea ofisini Kwao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri amesema kuwa moja ya vitu ambayo watanzania wanatakiwa kuvidumisha ni utalii wetu ili kuweza kuongeza pato la Taifa.

Amesema, kwenye baadhi ya sehemu ambazo zimesahaulika ni Utalii wa Utamaduni kitu kinachopelekea kupotea kwa tamaduni zetu ikiwemo vyakula, mavazi, sanaa za mkono na michoro, michezo pamoja na lugha ya Kiswahili.

Amesema, kuanzia mwaka huu wameweka mwezi Septemba kuwa mwezi wa Utamaduni utakaokuwa unajulikana kama Urithi Festival ambapo kutakuwa na maonesho mbalimbali ya vitu vya utamaduni ili kuvutia watu wa nje waje kujionea namna utamaduni wa watanzania ulivyo.















Hasunga amesema kuwa, lengo kuu la maonesho hayo ni kuongeza watalii nchini  ikiwemo na kuongeza mapato ya ntaifa kutoka Dola Bilioni 1.2 kwa mwaka na kuwa zaidi ya hiyo.




















'Tanzania ina vivutio vingi vua utalii ila vimekuwa vikiharibiwa na watanzania wenyewe na kusababisha Tanzania kushuka kutoka nafasi ya pili hadi ya nane kwenye vivutio vya utalii duniani unaotokana na uvamizi wa wakulima na uvamizi wa mifugo kwenye hifadhi za taifa," amesema













" Kwa sasa serikali inataka kuondoa mfumo wote na kurudisha hadhi ya hifadhi zote ili kuboresha utalii ikiwemo wa ndani kutokana na kushuka kutoka watalii laki nane  (800,000) kwa mwaka na kufikia watalii  laki sita na elfu ishirini na nne (602,400)," amesema Hasunga.













Hasunga amesema kuwa kumekuwa na utofauti mkubwa sana kulinganisha na nchi zingine katika kutembelewa na watalii ambapo kwa nchi kama Misri wamekuwa wanapokea watalii Milioni 10 kwa mwaka, Morroco wakipata watalii Milioni 13 huku Afrika Kusini wakipata watalii Milioni 1,500,000.













Akisisitiza zaidi, Naibu Waziri amewataka TTB kujitangaza zaidi kwa kila kivutio kilichopo kwenye mkoa, , kutumia Digital Market,  kutengeneza makala (video) zinazohusu vivutio, kuweka mabango barabarani ikiwezekana baadhi ya barabara wakabidhiwa kabisa Bodi hiyo.













Akijibu hoja za Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa  katika upande wa makala wapo katika hatua za kukamilisha na wanatarajia kuzindua mwakani mwezi Machi na utazinduliwa nchini Ujerumani.













Amesema kuwa, makala hizo zitaelezea zaidi kuhusu utalii wa ndani, hata hivyo matarajo ya kuongeza watalii wa ndani kwa kuongeza mabalozi ambapo wka sasa wana mabalozi tisa kutoka sehemu mbalimbali nchini.













Aidha, ameweka wazi msimamo wa TTB kwenye kutangaza utalii ikiwemo kutumia baadhi ya mashirika ya ndee kama Qatar, ligi kuu ya Uingereza na tayari makampuni mengine kama Emirates wapo kwenye mazungumzo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea bodi ya Utalii Nchini (TTB) na kuzungumza na menejimenti nzima na kuwataka kutanaza vivutio vya hapa nchini.







Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa na

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga na kumuahidi kutekeleza yale aaliyowaagiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad