WAHAMIAJI haramu 298 wamekamatwa mkoani Tanga kutoka nchi
mbalimbali ambao waliingia nchini kinyume cha kisheria na hivyo
kujikuta mikononi mwa vyombo vya dola.
Hayo yalisemwa na
Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga Ali Dady wakati akizungumza na mtandao huo
ofisini kwake kuhusu wahamiaji haramu waliokamatwa kwa kipindi cha
kuanza Januari hadi Agosti mwaka huu.
Alisema mwezi January
walikamatwa wahamiaji haramu 49 ambao walikuwa wametoka kwenye nchi
mbalimbali ikiwemo Somalia,Kenya,Tanzania na China huku kwa mwezi
February wakimatawa 77 kutoka nchi za Somalia,Ethiopia,
Burundi,Uganda,Kenya na Paskistani.
Afisa Uhamiaji huyo
alisema katika mwezi Machi na Aprili idadi yao uingiaji wa wahamiaji
hao ulishuka ambapo Machi walikamatwa 18 na Aprili walikamatwa 26 huku
mwezi Mei wimbi la ukamataji wao liliongezeka.
“Kwa mwezi
Mei walikamatwa wahamiaji haramu 94 kutoka kwenye nchi za Ethiopia,
Congo, China na Somalia huku mwezi June na Julai wakikamatwa wahamiaji
12 “Alisema.
Hata hivyo alieleza kwamba katika mwezi Agosti
mwaka huu walimatwa wahamiaji haramu 22 kutoka nchi za
Ethiopia,Kenya,Somalia na Tanzania ambao wamekuwa mawakala wa
wahamiaji hao.
Alisema idadi ya wahamiaji kuingia mkoani
Tanga imekuwa ikipungua kila wakati kutokana na kuwepo kwa ufuatiliaji
sambamba na kuwekwa vizuizi kwenye maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment