HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 4 October 2018

VODACOM YAWAKUMBUKA WATEJA WAKE WA SIKU YA KWANZA INAANZISHWA

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Harieth Lwakatale (kulia) akiwakabidhi zawadi baadhi ya wateja wa mtandao huo walio jiunga siku ya kwanza na yapili mtandao huo ulipoanzishwa nchini Tanzania. Wateja hao wa kwanza walipata fursa ya kutembelea na kujifunza shughuli za Vodacom Tanzania ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Harieth Lwakatale (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wa mtandao huo walio siku ya kwanza na yapili mtandao huo ulipoanzishwa nchini Tanzania. Wateja hao wa kwanza walipata fursa ya kutembelea na kujifunza shughuli za Vodacom Tanzania ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi akikata keki maalum ya kuwashukuru wateja kwa kuiamini kampuni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Harieth Lwakatale akishuhudia.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (kulia) akimuhudumia mmoja wa wateja aliyefika kupata huduma kituo cha Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi akizungumza kuwashukuru baaadhi ya wateja waliofika kupata huduma kituo cha Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi akigawa keki maalum wateja waliofika kupata huduma ofisi kuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam kama ishara ya shukrani kwa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

MTANDAO wa simu za mkononi Vodacom Tanzania imewakumbuka baadhi ya wateja wake waliojiunga siku ya kwanza na ya pili wakati mtandao huo ukianza kazi nchini Tanzania. Wateja hao wamepata fursa ya kutembelea shughuli mbalimbali zinazofanywa Makaao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania, kupewa zawadi pamoja na kupata fursa ya kuzungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ndugu Hisham Hendi.

Akizungumza mara baada ya wateja hao kukabidhiwa zawadi mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi aliwashukuru wateja hao kwa kuwa bega kwa bega na mtandao huo tangu kuanzishwa kwake na kuwahakikishia kampuni hiyo itaendelea kubuni huduma bora na nafuu kwa wateja wake.

Aidha aliwataka kuwa mabalozi wazuri wa Vodacom Tanzania kwa kuwa wao wamejifunza mengi kwa kutembelea shughuli za mtandao huo na kupata fursa ya kuuliza masuala mengi yanayofanywa na mtandao huo unaoongoza wa simu za mkononi nchini Tanzani. "...Tunawashukuru sana kwa kuwa na Vodacom tangu inaanzishwa hadi leo naomba muendelee kuwa mabalozi wetu, kwa mlichojifunza leo," alisema Hisham Hendi.

Katika tukio hilo, Hendi pia aliwahudumia wateja na kukata keki maalum kabla ya kuanza kuwagawia wateja wake waliokuwa wakiendelea kupata huduma kwenye duka la Vodacom na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo kilichopo Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Barabara ya Kawawa, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (kulia) akimuhudumia mmoja wa wateja aliyefika kupata huduma kituo cha Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wakipata picha ya pamoja na

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (wa nne kulia) walio tembelea kituo cha Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wateja wa mwanzo wa Vodacom Tanzania wakipata picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Harieth Lwakatale (kulia) (wa nne kulia) walio tembelea kituo cha Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad