HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 3, 2018

Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Doroth Gwajima akiangalia mtoto ambaye amezaliwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya Kitengo cha Wazazi Meta. Baadhi ya wajumbe wa Bodi na Maofisa wa NHIF walitembelea hospitali hiyo kuangalia huduma za wanazopata wanachama wake.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya na baadhi ya Vituo mkoani humo kwa lengo la kuangalia huduma wanazopata wanachama wake.

Katika ziara hiyo, ujumbe wa NHIF ulikutana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Wazazi Meta na Hospitali ya Uyole ambapo pamoja na mambo mengine walijadili juu ya huduma zinazotolewa kwa wanachama wa Mfuko.

Akiongoza ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bwana Tryphon Rutazamba alisema kuwa mbali na kujadili huduma lakini pia wamepata fursa ya kukagua mradi wa Jengo la Wodi ya Daraja la Kwanza inayojengwa pamoja na uzalishaji wa Maji tiba katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa fedha za Mkopo wa NHIF.

“Tumepita na kuangalia maeneo ambayo wanachama wetu wanapata huduma, tumeona pia wanachama na kuzungumza nao ambao wamekiri kupata huduma nzuri hivyo tunawapongeza hawa watoa huduma kwa jitihada kubwa za uboreshaji wa huduma ambazo wanazifanya,” alisems Bw. Rutazamba.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Fred Mbwanji aliushukuru Mfuko kwa kuboresha huduma zake lakini pia kwa fursa ya mikopo nafuu ambayo imewawezesha kuboresha kwa kiwango cha juu huduma za matibabu hospitalini hapo.

“Tunajenga Wodi ya Daraja la Kwanza kwa fedha ambazo ni mkopo nafuu kabisa kutoka NHIF, lakini pia tuna mradi wa kuzalisha Maji Tiba ambao ni mkopo pia kutoka kwenye Mfuko hivyo unaweza ukaona ni kwa namna gani NHIF imekuwa ni nguzo kubwa katika uimarishaji na uboreshaji wa huduma,” alisema Dkt. Mbwanji.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi Tryphon Rutazamba akimsalimia Mama na mtoto ambao ni wanachama wa Mfuko waliokuwa wamelazwa katika Hosptali ya Wazazi Meta, Mbeya.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Uyole Mbeya Dkt. Sijabaja akitoa maelezo kwa huduma anazotoa katika hospitali hiyo.
Wajumbe wa Bodi wakifurahia jambo mara baada ya kukagua jengo linalojenhwa kwa fedha za Mkopo kutoka NHIF katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Wajumbe wa Bodi wakiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dkt. Fred Mbwanji katika ukaguzi wa jengo linalojengwa kwa fedha za mkopo kutoka NHIF.
Mganga Mfawidhi wa Kitengo cha Wazazi Meta, Mbeya Dkt. Francis Rwegoshora akielezea huduma zinazotolewa katika kitengo hicho.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Wodi Daraja la Kwanza inayojengwa kwa kwa fedha za Mkopo kutoka NHIF.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bwana Rutazamba akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya.

1 comment:

  1. Hey, very nice site. I came across this on Google, and I am stoked that I did. I will definitely be coming back here more often. Wish I could add to the conversation and bring a bit more to the table,but am just taking in as much info as I can at the moment. Thanks for sharing.

    Wheelchair SM100.3


    ReplyDelete

Post Bottom Ad