HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 8 October 2018

TAMASHA LA WAJASILIAMALI KUFANYIKA OKTOBA 13 KINONDONI


CHAMA cha wajasiliamali Tanzania kinatarajia kufanya tamasha kubwa la wajasiliamali litakalofanyika Oktoba 13  mwaka huu kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutambulisha tamasha hilo Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka amesema kuwa tamasha hili litawasaidia wajasiliamali kuonyesha bidhaa  zao za mikono.

Pia amesema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na wajasiliamali mbalimbali watakao toa ushuhuda kuhusiana na ujasiliamali pia kutakuwa live bendi kutoka kwa msanii wa taarabu Isha Mashauzi.

Kiingilio cha tamasha hilo kwa viti maalumu VIP ni shilingi 40,000/= na viti vya kawaida ni shilingi 20,000/=

Nae Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha mwanamke wilaya ya ubungo Hidaya Njaidi amewaomba akinamama, akinababa pamoja na wanafunzi wa shule zote jijini Dar es Salaam kufika kwaajili ya kupata kile wajasiliamali wa jiji la Dar es Salaam walichowaandalia.
Mawasiliano kwaajili ya kujipatia kadi za kiingilio katika tamasha hilo  wasiliana na Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka namba o716589737 tigo au 0687935927 airtel.Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka akizungumza na MICHUZI BLOG wakati akitambulisha tamasha la wajasiliamali litakalofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam Oktoba 13 mwaka huu.
 Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha mwanamke wilaya ya ubungo Hidaya Njaidi jijini Dar es Salaam leo wakati walipotambulisha tamasha la wajasiliamali litakalofanyika Oktoba 13 Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha mwanamke wilaya ya ubungo Hidaya Njaidi akizungumza jijini Dar es Salaam leo na MICHUZI BLOG wakati akihamasisha wanawake na wananchi kwa ujumla kwenda kwenye tamasha la wajasiliamali litakalofanyika Oktoba 13 mwaka huu kinondoni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad