HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 20, 2018

SHIRIKA LA GREAT HOPE WATOA TUZO KWA WASHIRIKI WA UWEZO AWARD


 SHIRIKA la Great Hope Foundation leo limetoa tuzo kwa washiriki wa mradi wa UWEZO AWARD katika sherehe zilizofanyika chuo kikuu cha Dar es Salaam leo katika shule za Sekondari za hapa nchini.

 Mradi huu unaendeshwa kwa njia ya mashindano ambapo wanafunzi hushindana kutumia uwezo wao kufanya kazi mbalimbali za kijamii ambazo wao wanachagua kufanya.

UWEZO AWARD ina malengo makuu matano ambayo ni  Kuwatengenezea wanafunzi jukwaa la kujitambua/kufahamu uwezo/vipaji walivyonavyo ( hata vile ambavyo havionekani zaidi darasani.
, Kuwapa wanafunzi jukwaa la  kujifunza uongozi  Kuwapa wanafunzi jukwaa la kujifunza kuwajibika na kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayowazunguka
, Kutambua na kutoa tuzo kwa miradi bunifu iliyofanywa na wanafunzi katika UWEZO AWARD na  Kukuza na kuwajengea wanafunzi ujuzi katika maeneo ambayo wanafunzi wameonesha UWEZO.

Kwa mwaka 2018, Great Hope Foundation imeshirikiana na UN Tanzania, kufanya mradi huu wa Uwezo Award, kuwapa wanafunzi fursa ya kutambua kuwa jitihada wanazozifanya katika muda wao wa ziada kupitia UWEZO AWARD zinasaidia kuwapa ujuzi ambao una mchango mkubwa katika  kuyafikia malengo endelevu ya Dunia. UWEZO AWARD ina mchango wa moja kwa moja katika baadhi ya malengo haya endelevu ya Dunia kama

LENGO NAMBA 4; ELIMU BORA
 UWEZO AWARD inawapa wanafunzi kuendeleza uwezo wao, hata ule ambao hauonekani kabisa darasani, kama ambavyo imeainishwa na Haki za Watoto upande wa Elimu.

LENGO NAMBA NANE: KUBORESHA NA KUKUZA UCHUMI ENDELEVU WENYE KUTOA AJIRA NA KAZI ZENYE STAHA KWA WOTE
UWEZO AWARD inawapa fursa wanafunzi kujitambua na kupata ujuzi katika maeneo ambayo wao wanaona wanayapenda na kuyamudu, na huu ujuzi unawasaidia kupata ajira za moja kwa moja kwenye soko la ajira au kujiajiri wenyewe

LENGO LA TISA; KUJEGA MIUNDOMBINU IMARA; KUANZISHA VIWANDA ENDELEVU KUFANIKISHA NAKUSUKUMA MBELE UBUNIFU
 UWEZO AWARD inawajengea Wanafunzi kujiamini na kuwa wabunifu ambapo, ubunifu wanaoutumia katika kufanikisha miradi yao ya UWEZO AWARD, huwapa ujasiri wa kuanzisha miradi mbalimbali wanapotoka nje ya shule.

LENGO LA KUMI: KUPUNGUZA PENGO KUBWA LILILOPO KATI YA WATU WALIONA KIPATO NA MASKINI SANA
UWEZO AWARD inawajengea ujuzi wanafunzi, ambao wanautumia kama nyezo ya kupata ajira au kujiajiri na hivyo kuwasaidia kupunguza umaskini wa kipato wanapotoka nje ya shule.

Tunafurahi kuona wanafunzi walioanya mradi wa UWEZO AWARD 2017 wakitumia ujuzi na ujasiri walioupata katika UWEZO AWARD na kufanya miradi mbalimbali. Mfano wanafunzi wa WAILES Sekondari walipomaliza mradi wao, walianzisha mradi wa kutengeneza sabuni na kuuza, wakauita mradi wao ZUNGU na mpaka leo unaendelea. Wamefanikiwa pia kuanzisha mradi wa kusaga na kuuza karanga. Pia kuna mwanafunzi aliyetoka Zanaki aliyeshiriki UWEZO AWARD 2016, ambaye sasa anasoma Chuo na bado anaendeleza ndoto yake ya kuwa mbunifu wa mavazi.
  
Ndio maana tumefanya jitihada za kupeleka huu mradi nje ya Dar es Salaam na sasa tumefikia mikoa ya Morogoro na Pwani tukiamini wanafunzi wengi watanufaika zaidi. Na hadi sasa tumezifikia shule 100 katika mikoa hiyo ya Dar es salaam,Morogoro na Pwani.

Wanafunzi wamefanya miradi yao ndani ya miezi sita, yaani kuanzia mwezi wa tatu hadi wa nane.Mwezi Oktoba ( 20/10/2018) Tuzo zinatolewa kwa wanafunzi waliofanya miradi bunifu iliyokidhi vigezo na masharti tarajiwa.
Washindi wa kwanza wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo. Washiriki hao ambao ni kutoka shule ya sekondari ya Zanaki wamejinyakulia Tofi ya Silva pamoja na safari ya kutembelea mbuga za wanyama hapa nchini.
Washindi wa pili wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo.
Washindi wa tatu wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo.
  Washindi wa nne wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kidedea kwa kufanya vizuri zaidi katika mradi huo ulioendeshwa na shirika la Great Hope foundation jijini Dar es Salaam leo.










 Baadhi ya wanafunzi wakionyesha umahili wao katika michezo mbalimbali.



 Washriki ambao ni shule za sekondari 17 za jijini Dar esalaam wakiwa na vyeti vyao vya ushiriki.





 Washiriki mbalimbali wakipewa tuzo zao kutoka wa wawakilishi wa makampuni yaliyoshiriki katika kufanikisha uwezo Awads inafanikiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad