HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 4, 2018

SERIKALI YASIMIKA TAA ZA KUONGOZEA MAGARI MANISPAA YA MOROGORO


Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kikosi cha Umeme, imefanikisha mradi wa kufunga taa za kuongozea magari (Traffic lights) katika Manispaa ya Morogoro. Taa hizo za kisasa ambazo zinatumia nishati ya jua zimesimikwa katika makutano ya barabara ya Mei mosi na Korogwe inayotokea kituo kikubwa cha mabasi cha Msamvu kuingia mjini. 

Akizungumza wakati wa tukio la usimikaji wa taa hizo, Kaimu meneja wa Kikosi cha Umeme kutoka wakala huo Mhandisi Pongeza Semakuwa alisema mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni mia moja na sitini na sita na ni wa kwanza kufanywa na wakala katika manispaa hiyo, ‘’taa hizi ni za kisasa zaidi na zinatoa suluhisho la muda kwa watumiaji kwakua zinahesabu sekunde mtumiaji akiwa anaona, tupo kwenye majadiliano na TARURA na kuna uwezekano tukasimika taa katika maeneo mengine hapa,’’ alisema Mhandisi Pongeza.

Aidha Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Manispaa ya Morogoro Mhandisi Mnene James amesema wataendesha mafunzo wakishirikiana na TEMESA kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hizo kuhusu namna sahihi ya kutumia taa hizo na alama za kivuko cha waenda kwa miguu ili kuepusha ajali ambazo zimekua zikitokea mara kwa mara katika eneo hilo hasa kwa madereva wa bodaboda. 

Kukamilika kwa mradi huo kunaifanya Manispaa ya Morogoro kuwa na makutano ya pili kuwekwa taa za kuongozea magari baada ya makutano ya barabara ya Mazimbu na Iringa eneo la Tumbaku kupitiwa na mradi kama huo hivi karibuni.
 Muonekano wa taa za kuongozea magari (traffic lights) zilizosimikwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika manispaa ya Morogoro katika makutano ya barabara ya Mei mosi na Korogwe inayotokea kituo kikubwa cha mabasi cha Msamvu kuingia mjini. Taa hizo za kisasa zinatumia umeme wa jua.
 Mafundi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifunga taa za kuongozea magari (traffic lights) katika makutano ya barabara ya Mei mosi na Korogwe manispaa ya Morogoro. Kukamilika kwa mradi huo kunaifanya Manispaa ya Morogoro kuwa na makutano ya pili kuwekwa taa za kuongozea magari baada ya makutano ya barabara ya Mazimbu na Iringa eneo la Tumbaku kupitiwa na mradi kama huo hivi karibuni.
 Fundi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) akiunganisha nyaya katika paneli ya sola itakayotumika katika kuongozea mfumo wa taa za kuongozea magari zilizosimikwa katika makutano ya barabara ya Mei mosi na Korogwe manispaa ya Morogoro.
 Kaimu meneja wa Kikosi cha Umeme kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Pongeza Semakuwa kulia akikadiria na kuseti sekunde katika kidhibiti muda (‘’controller’’) ya kuongozea taa za barabarani ambazo zimesimikwa katika manispaa ya mji wa Morogoro katika makutano ya barabara ya Mei mosi na Korogwe.
Mafundi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiweka boksi la kuhifadhia kifaa cha kudhibiti na kukadiria muda wa kuwaka kwa taa za kuongozea magari barabarani (‘’controller’’), taa hizo zimesimikwa katika manispaa ya mji wa Morogoro katika makutano ya barabara ya Mei mosi na Korogwe. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad