Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
Tanzania Red Cross imezindua kampeni ya mafunzo ya kutambua matumizi nembo za Red Cross kutokana na baadhi ya watu au Taasisi kutumia nembo hiyo wakati hawana mamlaka ya kutumia nembo hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Julius Kejo amesema kuwa uzinduzi wa kampeni hiyo ni kuwajuza wananchi kuhusiana na nembo hiyo juu inavyotumika na Red Cross na hakuna mtu yeyote anayeruhusiw kutu,ia nembo.
Kejo amesema kuwa nembo ya Red Cross kwa nchini wanaweza wakawa wanatumia bila kujua kuwa hawana mamlaka ya kutumia nembo hiyo ni kwa ajili ya kulinda masilahi ya nembo hiyo isijekatumika katika masuala ya uhalifu na kuondoa maana ya Red Cross.
Kejo amesema kampeni hizi zitatoa mafunzo jinsi ya matumizi kwa ujumla duniani kote hivyo basi ni jukumu la kila mtu kuilinda nembo hiyo
Katibu Mkuu huyo amewaasa wanahabari kufikisha ujumbe kwa watu,taasisi pamoja na mashirika binafsi ambao wamekua wakitumika biaadhi ya nembo hizo kuwa si sheria kutumia nembo hizo.
Kejo amesema Red Cross kazi ya Red Cross ni kukabiliana maafa, kuelimisha jamii kuhusu kujikinga na majanga mbalimbali ili kupunguza madhara ya majanga hayo pamoja na kuunganisha wanafamalia na ndugu waliopotezana wakati wa majanga au matatizo mengine ya kijamii.
Aidha amesema kazi ya Red Cross ni pamoja na kutoa huduma ya kwanza kwenye mikusanyiko ya watu kama vile wakati wa michezo,mikutano,matamasha.
Kejo amesema kampeni hiyo itaambatana na majukwaa mbalimbali ,vipeperushi,mitandao ya kijamii ikiwa ni dhamira ya kusambaza elimu kwa jamii ili kuepuka matumizi mabaya ya nembo hizo
Mwakilishi kutoka nchi ya Hispania wa Red Cross Andrea Heath amesema kuwa kampeni hiyo ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuhusiana na nembo za Red Cross kuwa huwazitumiki na watu binafsi isipokuwa kuna vyombo vinavyotumia nembo hiyo kama majeshi.
Katibu Mkuu wa Red Cross Tanzania Julius Kejo akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua kampeni kuelimisha kuhusiana na nembo ya Red Cross uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Malengo wa Kamati ya Red Cross Kimataifa Andrea Heath akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchango wa Red Cross katika majanga mbalimbali.
Mwakilishi wa Red Cross kutoka nchini Hispania Monica Cardena akizungumzia kuhusiana na kazi za Red Cross.
Nembo za Red Cross ambazo ndizo zinazotumika
No comments:
Post a Comment