Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari leo kufungua
rasmi pazia la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote litakalofanyika jumamosi hii uwanja wa CCM Kirumba Mkoani
humo. Wengine pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa,Uthman Madati na Msanii Nikki
Wa Pili.
Mkuu wa Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane kilichopo mkoani Mwanza, Beatrice Kessy akizungumza na
waandishi wa habari na Wasanii watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta kesho jumamosi kuhusu umuhimu
wa watalii na watanzania kutembelea kisiwa hicho.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthman Madati akizungumza na Waandishi wa habari leo kwenye
mkutano wa uzinduzi wa Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, Msanii Nikki wa Pili na Meneja wa Masoko Tigo Mkoa
wa Mwanza, Kassimu Azziz.
Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Tigo na wasanii wataopanda kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa CCM Kirumba kesho.
Jumamosi hii, jiji la Mwanza linatarajiwa kufurika na vibe kama
lote kutoka kwa wasanii 100% wanaokonga nyoyo za mashabiki wa msimu huu wa Tigo Fiesta
2018- Vibe Kama Lote.
Baada ya wiki saba ambazo zimeshuhudia msimu huu mkubwa zaidi wa kitamaduni katika
ukanda wa Afrika ya Masahariki na Kati ukizuru miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa,
Njombe, Mtwara, Songea na Moshi, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote sasa imetua katika
fukwe za Ziwa Victoria na ipo tayari kutifua vumbi katika viwanja vya CCM Kirumba leo
Jumamosi tarehe 27 Oktoba.
Waandaaji wa tamasha hilo, kampuni ya Clouds Media group wamesema vibes katika jiji la
Mwanza zitaongozwa na msanii Fid-Q ambaye ni mzaliwa wa jiji hilo, akisindikizwa na kundi la
Weusi, Rostam, Wakazi na Rich Mavoko. Wasanii wengine watakaopagawisha siku hiyo ni Jux,
Barnaba, Whozu, Nandy, Aslay, Country Boy, Nedy Music, Nkunda Star pamoja na Jay Melody.
Mwanza pia itashuhudia vibes kutoka kwa Mchama the Best, Jolie, Benson watakaotanguliwa
na washindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota.
Akiashiria kuanza kwa msimu huu wa vibes jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella alizungumzia uwepo wa fursa za biashara zinazoambatana na msimu huo. “Wamiliki
wa kumbi za starehe, hoteli na nyumba za kulala wageni, mam ntilie, wauza maji na wamiliki wa
vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda wote wana fursa kubwa ya kujiongezea kipato kwa
sababu tunaratajia maelfu ya wageni kufurika jijini Mwanza katika kipindi hiki,’ alisema.
Hali kadhalika, kampuni ya Tigo imewakumbusha wakaazi wa Mwanza wazikose kufurahia
promosheni murwa ya Data Kama Lote itakayowapa bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi
vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja
wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’
Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018
zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Mwanza litakalofanyika,
tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 8,000 pekee
badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga
*150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na
kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na
msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.
Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni,
simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH
milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda
15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote
ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi.
Baada ya Mwanza, tamasha hilo linahamia Musoma kabla ya kutua Muleba, Kahama, Arusha
Singida na Dodoma, huku kilele kikifanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment