HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 October 2018

Mvua kwa mikoa ya Pwani na Dar kuanza Novemba mwaka huu

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MAMLAKA ya hali ya Hewa nchini,( TMA) imesema mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.
Pia TMA imetoa utabiri wa msimu wa mvua wa kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 kwa mikoa inayopata mvua Mara moja kwa mwaka ambazo zinatarajiwa kuwa za juu na wastani.
Akizunguza wakati akitoa utabiri huo, jijini Dar es Salaam leo Oktoba 18, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Agnes Kijazi amesema mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kisini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara. Huku maeneo ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songea yakitarajiwa kuata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
"Kutokana na mifumo ya Hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka, maeneo yaliyosalia ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Amesema, mvua za msimu ni mahususi kwa maeneo ya magharibi mwa nchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.
Aidha Kijazi amezitaka sekta mbalimbali zinazotumia taarifa ya hali ya hewa katika kutekeleza majukumu yao kama vile, kilimo na usalama wa chakula, Afya, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, uchukuzi na Mawasiliano, Nishati, Maji na nyingi za kuchukua taathari kufuatia mvua hizo nyingi kwani inaweza kusababisha madhara mengi katika Jamii nzima.
 Kwani matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza kupelekea maji kutuama na kusababisha mafuriko.
 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu utabiri wa msimu wa mvua wa kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 kwa mikoa inayopata mvua Mara moja kwa mwaka ambazo zinatarajiwa kuwa za juu ya wasatani na wastani leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad