HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 13 October 2018

MAONESHO YA SITE KUCHAGIZA UKUAJI WA SOKO LA UTALII DUNIANIMoja ya washiriki wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo akiangalia baadhi ya bidhaa zilizoteneznezwa na wajasiriamali wadogo wadogo katika maonesho yaliyoanza jana Oktoba 12 na kumalizika Oktoba 14.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAONESHO ya Kimataifa ya Utalii nchini Swahili International Tourism Expo (SITE) yatanua wigo wa utalii kwa wageni kutoka nje ya nchi.

Maonesho hayo yaliyoanza jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere yamekuwa yameleta chachu ya ongezeko la watalii wa ndani na nje ya nchi. 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema maonesho ya utalii ni muhimu katika ukuaji wa sekta ya utalii nchini. 

Onesho la S!TE ni onesho la utalii linalomilikiwa na Bodi ya Utalii Tanzania linalofanyika kila mwaka mwezi Oktoba. Onesho hili lilianzishwa mwaka 2014, hivyo ni mara ya nne kwa onesho hili kufanyika. 

Devotha amesema kufanyika kwa onesho hili ni moja ya utekelezaji wa jukumu letu kuu la kuitangaza Tanzania kama eneo bora duniani kwa safari za kitalii, mapumziko, mikutano na maonesho. 

Amesema kuwa kwa mwaka huu nchi zinazoshiriki zimeongezeka na kufikia nchi 44, Idadi ya Kampuni nayo imeongezeka na kufikia 170 na mawakala wa utalii walioalikwa kutoka nchi mbalimbali ni 300. 

"Kwa mwaka huu, maonesho yamegawanyika katika makundi tofauti ambazo ni Kampuni ya wasafirishaji watalii, Wakala wa usafiri wa anga, watoa huduma za malazi, vikundi vya utalii wa Kitamaduni, waandaji wa utalii wa mikutano, wasanii wa sanaa za mikono, Waongoza watalii, Mashirika ya ndege, idara na Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, na watoa huduma nyingine katika sekta ya utalii, "amesema Devotha. 

Devotha amesema lengo kubwa la maonesho haya ni kuwawezesha washiriki toka nchini kukutana na mawakala wakubwa wa utalii toka maeneo mbalimbali duniani na kutoa fursa kwa wao kuingia makubaliano ya kibiashara. 

Ameeleza kuwa Ili kuwapa Wakala hao toka nje ufahamu mzuri wa utalii wetu tumewaandalia pia ziara ya kutembelea maeneo mbalimbnali ya vivutio mara baada ya onesho kumalizika. 

Baadhi ya maeneo watakayotembelea ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa, na Tarangire, bonde la Ngorongoro, visiwa vya Zanzibar na Mafia pamoja na fukwe ya Pangani.Aidha onesho hili pia hutumika kama fursa ya kutangaza Utalii wa ndani ambapo watoa huduma za Utalii wa Tanzania huweza kuhamasisha wageni wanaotembelea onesho la S!TE kutumia huduma zao na kutalii sehemu mbalimbali nchini pamoja na kujifunza fursa mbalimbali za sekta ya utalii. 

Aidha, Katika kuviwezesha vikundi vidogo vidogo (yaani SMEs), wakina Mama, na watu wenye ulemavu TTB iliona ni vyema kuyashirikisha makundi kadhaa kwa kuyapa fursa ya kuandaa sare, mifuko na zawadi maalum za wadhamini. Kati ya watu wanaotoka katika makundi haya walioshiriki kikamilifu ni Mshonaji Maarufu nchini, Dkt. Abdallah, ambaye ana ulemavu 

wa macho na Bwana Rubuni mchongaji maarufu wa Sanaa ya Tinga Tinga.

Mdau akipata maelezo kutoka kwa mshiriki wa
maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini Swahili International Tousrim Expo (SITE) 
Mataifa mbalimbali yakiwa yamekuja kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini Swahili International Tousrim Expo (SITE). 


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad