HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 18, 2018

MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za kimahakama wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Happyness Ndesamburo.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na viongozi wengine wa Mahakama pamoja na Mahakimu wa Mahakama zilizopo wilayani Kwimba mara baada ya kuzungumza nao.
.Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga pamoja na Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Mansoor Shanif Hiran.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kwimba baada ya kuzungumza nao leo katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika.

 Na Lydia Churi-Kwimba Mwanza 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakumbusha  Majaji na Mahakimu kutumia Mamlaka waliyonayo kisheria kutoa adhabu zinazoirekebisha jamii kwa makosa yanayojirudia mara kwa mara.
Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kwimba leo Jaji Mkuu alisema Mahakama ni sehemu ya jamii hivyo inalo jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani na salama.
Kuhusu ushirikiano kati ya Mahakama na mihimili mingine, Jaji Mkuu alisema katiba ya nchi imegawanya majukumu kwa kila mhimili lakini yote inaunganishwa  na dhana moja ya kuwatumikia wananchi, hivyo aliahidi kuendeleza ushirikiano na wadau wote ili wananchi wapate haki kwa wakati.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama haiwezi kufanya kazi peke yake bila kushirikiana na mihimili mingine. “Nguvu ya Mahakama inatokana na nguvu kutoka kwenye mihimili mingine”, alisema.  
Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi  Ngaga alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao hulazimika kukatisha masomo yao.
Kuhusu ushirikiano na Mahakama, Mkuu huyo wa wilaya alisema ofisi yake inashirikiana kwa karibu na Mahakama katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake katika mkoa wa Mwanza ambapo anakagua shughuli za Mahakama. Tayari ameshatembelea baadhi ya Mahakama zilizopo kwenye  wilaya za Ukerewe, Sengerema na Kwimba.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad