HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 5 October 2018

MAHAKAMA YA RUFANI JIJINI DAR YATUPILIA MBALI RUFAA YA VIONGOZI TISA WA CHADEMA


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5.2018 imetupilia mbali Rufaa iliyofunguliwa na viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wake Freeman Mbowe kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu dhidi ya mwenendo wa kesi ya uchochezi unayowakabili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu sababu taarifa ya kusudio la kukata rufaa hiyo inamapungufu kisheria.

Mapema mwaka huu, Mahakama kuu ilitupilia mbali maombi ya viongozi hao ya kutaka kufanya marejeo mwenendo wa kesi hiyo kwa sababu ya kuwepo mapungufu kisheria.

Rufaa hiyo ni mwendelezo kutokana na kesi ya msingi ya jinai inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo wanapinga uamuzi na amri mbalimbali ambazo mahakama hiyo imekuwa ikizitoa.

Uamuzi dhidi ya rufaa hiyo iliyoandaliwa na jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Mbarouk Mbarouk, Shaban Lilla na Jacobs Mwambegele,imesomewa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Eddy Fusi

Katika uamuzi huo, jopo hilo la Majaji limesema taarifa ya kusudio la kukata rufaa ya waombaji hao haielezi ni sababh au amri ipi wanayoitakatia rufaa kisheria.

Jopo hilo la Majaji limeeleza kukubaliana na Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 68(2) ya kanuni ya Mahakama ya rufaa, kuwa rufaa hiyo inamapungufu kisheria kwa kuwa waleta maombi hawaelezi ni amri ipi wanayoikatia rufaa kwani waombaji kwenye taarifa yao ya kukata rufaa wameeleza kuwa wanakatia rufaa uamuzi wote wa mahakama Kuu.

" mapungufu haya yanaenda kinyume na kanuni hiyo sababu kwenye mashauri ya jinai, taarifa ya kukata rufaa ndio inayoanzisha rufaa na kwa vile rufaa hii inamapungufu basi rufaa iliyopo mahakamani haiwezi kusimama na kwa sababu hiyo rufaa hiyo pia imefutwa.

Kutokana na hatua hiyo, imetupilia mbali rufaa ya vigogo hao 9, pamoja na kuyaondoa maombi ya kutaka kusitisha mwenendo wa kesi yao inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji, manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Pia wamo Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12 ambayo ni kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali yanayowakabili wote, huku Mbowe, Msigwa Mdee na Heche kila mmoja peke yake akikabiliwa na mashataka zaidi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 16 katika barabara ya Kawawa, Mkwajuni, Kinondoni, siku wakihitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni na kusababisha vurugu zilizosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad