HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 30 October 2018

MAHAKAMA KUTAJA TAREHE YA KUSOMEWA HUKUMU KWA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema Novemba 16, 2018 itataja tarehe ya kusomwa kwa hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Hatua hiyo imefikiwa leo Oktoba 30, 2018 baada ya mshtakiwa Mhando kupitia wakili wake Martin Matunda kuitaarifu mahakama kuwa wamefunga ushahidi dhidi ya kesi hiyo ambayo mshtakiwa Mhando amejitetea mwenyewe.

Aidha mahakama imewataka pande zote mbili, upande wa serikali na ule wa utetezi kuwasilisha hoja za majumuisho ya mwisho ya kesi hiyo Novemba 15, 2018.

Kabla ya kufungwa kwa kesi, akihojiwa na wakili wa upande wa mashtaka kutoka Takukuru Leornad Swai, Mhando amedai kuwa mchakato mzima wa kuingia ubia wa kuhamisha TBC kutoka mfumo wa analogia kwenda Digitali ( Star times) ulifanywa na bodi ya TBC.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Mhandi amesema hakuna kitu alichofanya bila ridhaa ya bodi, kwani bodi ndiyo iliniagiza nifanye mchakato wa awali na ulipokamilika niliwasilisha kwao mwaka 2009 na mpaka naondoka TBC hakuna mtu aliyezungumzia suala hilo la mkataba siyo Serikali wala bodi hiyo.

Alipoulizwa juu ya tofauti za mkataba aliongia na Chanel 2 na ule wa Startimes Mhando amedai, yeye aliandikishiana mkataba wa makubaliano na Chanel 2 kwa sababu walitaka kuhakikishiwa kama wangeitwa na bodi ya TBC ambao aliusaini yeye peke yake hukumkataba halisi waliingia na Star times ambao alisaini yeye Mhando na Mwanasheria.
"Mkataba wa Startimes ndiyo mkataba halisi ambao tuliandikishiana baada ya bodi kurudhia". Amedai Mhando.
Amesema kutokana na sheria na taratibu za manunuzi mkataba halali lazima usainiwe na watu wawili ambao ni Mkurugenzi na Mwanasheria na pia lazima uwena muhuri wa shirika.

 Mkataba wa makubaliano ya awali baina  ya TBC  na kampuni ya Channel 2 group ya Dubai niliusaini mimi kama Tido kwa kuwa walikuwa wanataka kuthibitishiwa.

Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka ambao wametoa ushahidi  katika kesi hiyo ni  Afisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana huku kwa upande wa utetezi, mashtakiwa Mhando amejitetea Mwenyewe.

Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh. Milioni 887.1

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad