HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 4, 2018

KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI KISARAWE KUTANUFAISHA SEKTA YA VIWANDA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyenge amesema kuwa kukamilika kwa mradi wa Kisarawe kutanufausha mji mzima wa kisarawe, eneo la sekta viwanda na vitongoji jirani na mji huo.

Akiwa katika awamu ya kwanza ya ziara ya siku 2 Pia aliongozana na Mwenyekiti wa kamati ya Bodi ya Ufundi Mhandisi Gaudence Aksante sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja

Akizungumza  baada ya kumaliza ziara ya siku ya kwanza, Jenerali Mwamunyange amesema kuwa mradi huo ukikamilika shida ya maji ya miaka mingi inakwisha chini ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

 Jenerali Mwamunyange amesema kuwa, DAWASA ina dhamira ya  kufikisha maji Kisarwe na kuondokana na uhaba wa upatikanaji wa maji kama agizo la Rais alivyoagiza wakati wa uzinduzi wa mtambo wa Ruvu Juu uliopo Mlandizi  mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo, Jenerali amejionea hatua miradi ya maji ilipofikia  na lengo zaidi ni kuongeza maji katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani na wananchi wawe na matumaini kwani mradi huo utakamilika ndani ya muda mfupi  na utapeleka maji lita 4,080,000 kwa siku.

Jenerali amesema, kulikuwa na changamoto ya kuendelezwa kwa miradi na mingine ikikaa mda mrefu zaidi ila DAWASA wameweza kukaa chini na wakandarasi na wamewahimiza kuhakikisha wanamaliza miradi hiyo kwa wakati na zaidi matatizo yao yametatuliwa.

Amesema, "nafahamu Jiji la Dar es Salaam linakua kila siku na kwa kila mwaka asilimia 5.7 ongezeko la wakazi na linakuwa na maji yanahitajika kwa wingi,"

Amemalizia kwa kuwekea msisitizo, kuwa DAWASA kupitia kwa menejimenti yake na Bodi wana mikakati ua kutafuta vyanzo vipya vya maji ili  kuongeza maji katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Dar es Salaam, kuboresha miundo mbinu iliyochakaa na ile inayovuja.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa mradi huo wa matanki yaliyojengwa sehemu tofauti yatasaidia ongezeko la wateja Milioni 1 wapya.

Amesema kuwa, mradi wa Salasala umeshatandikwa Km40 kwa ajili ya kuanza kuunganisba maji katika maeneo ya Madale, Changanyikeni, Mivumogi na Goba na zaidi changamoto kubwa ilikuwa ni mtandao kuwa mdogo na maji kuwa mengi.

DAWASA kwa siku inazalisha maji Lita Milioni 502 kwa siku.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyenge akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutembelea miradi mbalimbali ya maji inayosimamiwa na Mamlaka hiyo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuelezea jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyenge pamoja naMwenyekiti wa kamati ya Bodi ya Ufundi Mhandisi Gaudence Aksante sambamba wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyenge (katikati( akishuka ngazi katika moja ya Tanki lilijojengwa kwa ajili ya kuhifadhi maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad